Tanzia : MHASIBU MKUU MWANZILISHI WA STAND UNITED EMMANUEL 'LONDON SHOP' AFARIKI DUNIA


Mhasibu Mkuu Mwanzilishi wa Timu ya Stand United 'Chama la Wana" Emmanuel Mlimandago Dominic maarufu "London Shop" amefariki dunia leo Jumapili Februari 17,2019 saa moja asubuhi.

Kwa Mujibu wa rafiki kipenzi wa Emmanuel bwana Kennedy Nyangi ameiambia Malunde1 blog kuwa rafiki yake amefariki dunia leo asubuhi  katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza.

"Ni kweli ndugu yetu,rafiki yetu, Mwanachama wa Stand United amefariki dunia,alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya figo,msiba upo nyumbani kwa baba yake Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga",amesema Nyangi.

Itakumbukwa kuwa Emmanuel Mlimandago ni miongoni mwa waasisi wa Stand United na mwaka 2015 aligombea udiwani katika kata ya Ngokolo kupitia CCM akichuana na Emmanuel Ntobi (Chadema) ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.

R.I.P Emmanuel Mlimandago Dominic


Jumatatu Oktoba 12, 2015: Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo (katikati) akimnadi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele (kulia) na mgombea udiwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Mlimandago Dominic (kushoto).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post