Sunday, February 17, 2019

BASI LA GREEN LINE LAUA WATU 10 BAADA YA KUGONGANA NA LORI

  Malunde       Sunday, February 17, 2019

Watu 10 wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea katika barabara ya Nakuru- Eldoret kati ya basi la abiria la Green Line  na lori ya mizigo.


Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana leo Jumapili, Februari 17 katika eneo la kwa Harun, Kamara Nakuru. 

 Akithibitisha tukio hilo, chifu wa kata ya Kamara Joseph Korir alieleza kuwa watu wanane walifariki papo hapo huku wengine wawili wakifariki hospitalini walikokuwa wakipata matibabu. 

Madereva wa magari hayo mawili ni kati ya waliofariki kufuatia ajali hiyo.

Jumla ya watu 74 waliohusika katika ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali za Molo na Koibatek kwa matibabu.

Wanafunzi waliofunga shule kwa likizo fupi ni kati ya waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea siku moja tu baada ya ajali nyingine mbaya kufanyika katika barabara ya Kericho - Nakur.u eneo la Chepsir ambako watu watano walipoteza maisha.

Wakenya wamewalaumu vikali maafisa wa trafiki kwa ulegevu kazini ma kuutaka kama chanzo cha visa vya ajali ambavyo vimeonegezeka nchini. 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post