MCHUNGAJI AZUA GUMZO BAADA KUDAI KUMFUFUA MTU


Mchungaji Alph Lukau wa kanisa la Aleluia Ministry la Afrika Kusini amezua gumzo baada ya kudai kumfufua mtu wakati wa ibada yake ya Jumapili ya Februari 24,2019.


Mchungaji Alph Lukau  amezua mtafaruku mkubwa mitandaoni baada kudai amemfufua mtu, aliyeletwa na mwenye nyumba wake akidai kuwa alifariki baada ya kumkimbiza hospitali alipoumwa, na ndipo akaamua kumpeleka kanisani kumuombea.

Imeelezwa kuwa mtu huyo aliyedaiwa kufariki tangu Ijumaa alikuwa akipumua ndani ya jeneza.

Wananchi wameitaka serikali iwazuie wachungaji hao wanaowahadaa wananchi kwa miujiza.

Baada ya kusambaa kwa habari za Mchungaji wa Afrika Kusini Alph Lukau kumfufua mtu  kampuni inayouza masanduku ya mazishi (jeneza) imejitokeza na kusema kuwa sanduku hilo halikutoka kwao, na pia wanafikiria kumshtaki mchungaji huyo.

Akizungumza na Television ya SABC nchini Afrika Kusini, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya mazishi ya Kings and Queens, Mis. Vivian Mponda, amesema kwamba wao walifuatwa na mmoja wa wanafamilia wakiomba kutumia usafiri, lakini sanduku lililotumika halikuwa la kwao na wala mwili huo haukuhifadhiwa hapo kama wanavyodai, kwani huwa hawahifadhi mwili bila taarifa rasmi.

“Hatukuwauzia sanduku hivyo sio la kutoka Kings & Queens na hatuna sanduku la vile kwenye mochwari yetu, ila gari walikodi kwetu wakisema wanataka kulitumia kwenye mazishi ya ndugu yao”, amesema Ms. Vivian.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji (SABC) habari zinasema kwamba waandishi walimfuatilia mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Eliot na mpenzi wake ambaye alikuwepo siku ya tukio (kufufuliwa), na kugundua kuwa waliondoka nyumbani kwao tangu Jumatano, na hawajarudi mpaka sasa.

Wakiendelea kuchunguza hilo imebainika kuwa hata mtu aliyesema amempangisha nyumba yake ambaye ndiye alimfia mikononi sio kweli, kwani mwenye yeye ni mwanamke na aliyekuwepo siku ya tukio hilo alikuwa ni mwanaume.

TAZAMA VIDEO <<HAPA>> 




TAZAMA PICHA






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527