FATUMA KARUME : NAACHIA NGAZI TLS


Fatuma Karume, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) hatogombea tena nafasi hiyo baada ya kustaafu Aprili mwaka huu. 

Karume, mwanasheria huyo mwiba kwa Serikali ya Awamu ya Tano na mtoto wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Mstaafi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zabzibar ameeleza kuwa, nguvu kubwa baada ya kumaliza muhula wake wa mwaka mmoja ulioanzia Aprili mwaka jana, itakuwa ni kwenye biashara zao.

Katika orodha ya wanachama wa chama hicho waliojitosa kugombea nafasi hiyo, jina la Karume halikuwemo na alikuwa hajatoa maelezo yoyote.

Ikiwa leo ni tarehe 18 Februari 2019, zimebaki siku tatu kuhitimisha muda uliowekwa na kamati ya uchaguzi wa kuorodhesha majina ya wataowania nafasi hiyo. Kamati hiyo ilieleza mwisho kuwa tarehe 20 Februari 2019 (Jumatano wiki hii) saa 11 jioni.

“Baada ya kumaliza muda wangu wa mwaka mmoja, sitagombea tena. Naelekeza nguvu kwenye biashara zetu,” amesema Karume alipozungumza na mtandao huu na kuongeza;

“Jamaa zangu wamenishauri vizuri kuwa, niwekeze zaidi muda wangu kwenye biashara zetu.”

Karume ndio rais wa kwanza wa TLS mwanamke tangu kuanzishwa chama hicho mwaka 1954 kupitia Sheria ya Bunge ya mwaka 1954 (The Tanganyika Law Society Ordinance 1954).

Katika uchaguzi wa mwaka jana wa TLS, Karume ndiye mgombea aliyejitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi hiyo ambapo alimbwaga Godfrey Wasonga, Godwin Ngwilimi na Godwin Mwapongo.
Chanzo- Mwanahalisionline

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post