Picha : AGPAHI YATOA MSAADA WA KISAIKOLOJIA KWA VIJANA KUPITIA BONANZA LA MICHEZO MWANZA


Vijana wametakiwa kutokata tamaa,kuondoa hofu na kuwa makini katika maisha licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili waweze kufikia ndoto zao za maisha.Ushauri huo umetolewa Februari 23,2019 na Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu wakati wa Bonanza la Michezo lililokutanisha vijana kutoka kwenye klabu za vijana kutoka halmashauri za wilaya za Misungwi,Nyamagana,Sengerema na Kwimba mkoani Mwanza.

Klabu hizo zinasimamiwa na asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC).

Akifungua Bonanza hilo,lililofanyika katika Viwanja vya Lessa Garden Hotel jijini Mwanza, Olotu aliwashauri vijana kujiamini na kutokubali kukata tamaa lakini pia kuwa wasikivu wanapoelekezwa mambo ya msingi katika maisha.

“Kupitia michezo hii mmefurahi pamoja, mmefahamiana,mmepata marafiki wapya na kujifunza mambo kadha wa kadhaa kupitia michezo,naomba muendelee kujiamini na kuzingatia ushauri mnaopewa ili mtimize ndoto zenu, ni vyema pia kuwa wamoja na kuendelea kushirikiana”,aliongeza Olotu.

Kwa upande wake, Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona alisema AGPAHI imekuwa ikiandaa michezo kwa watoto na vijana ili kuwapa msaada wa kisaikolojia kwani asasi hiyo inajali watoto ili wakue na kuishi katika matumaini chanya.

Alisema bonanza hilo limeshirikisha vijana balehe zaidi ya 50 kutoka kwenye vituo vya tiba na matunzo kwenye halmashauri za wilaya mkoani Mwanza lengo likiwa ni kujifunza kwa njia ya michezo kuimarisha afya zao.

Miongoni mwa michezo iliyofanyika wakati wa bonanza hilo ni kukimbia mita 100,mbio za magunia,kabute,landrover na mchezo wa kufunga vitambaa usoni.

ANGALIA PICHA WAKATI WA BONANZA
Muuguzi mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akifungua bonanza la michezo lililokutanisha vijana kutoka kwenye klabu za vijana kutoka halmashauri za wilaya za Misungwi,Nyamagana,Sengerema na Kwimba mkoani Mwanza - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akiwahamasisha vijana kuwa wamoja na kushirikiana sambamba na kutokata tamaa ili wafikie ndoto zao za maisha. Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona.Wa kwanza kushoto ni Pudensia Mbwiliza na Joan John ambao ni Walimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akielezea malengo ya bonanza la michezo ambayo ni kuburudika na kujifunza kwa njia ya michezo.
Vijana wakicheza kwa kushika vichwa wakati wa bonanza hilo.
Mchezo wa Landrover ukiendelea.
Vijana wakiunga mstari kumfuata mshindi katika mchezo wa karatasi,jiwe na mkasi.
Vijana wa kike wakichuana kwenye mbio za mita 100.
Mchezo wa mbio za mita 100 ukiendelea kwa vijana wa kiume.

Mbio za magunia zikiendelea.


Mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo : Kulia ni Mwalimu wa vijana Douglas Renatus kutoka hospitali ya rufaa Bugando akitoa maelekezo kwa washiriki juu ya mambo ya kufanya huku wamefungwa vitambaa usoni.
Washiriki wa mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo wakiendelea kutembea huku wakipewa maelekezo kutoka kwa vijana waliowazunguka.
Mshiriki wa mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo baada ya kuvuka kikwazo namba mbili akichukua zawadi ya limao.

Watu wazima nao hawakubaki nyuma katika michezo hiyo ili kuwatia moyo vijana.
Mwalimu wa vijana Pudensia Mbwiliza akiwasisitiza vijana kutokata tamaa na kuepuka hofu katika maisha.
Mwalimu wa vijana Joan John akiwafurahisha vijana.
Vijana wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akitoa mwongozo wa kugawa zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika pamoja na zawadi za jumla kwa washiriki. Wa kwanza kushoto ni Nicholaus Michael na Douglas Renatus ambao ni walimu wa vijana kutoka hospitali ya rufaa Bugando. Kulia ni Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu.
Mshindi wa mbio za mita 100 kwa vijana wa kike akipokea zawadi ya saa kutoka kwa mgeni rasmi Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu. Wa kwanza kulia ni Mwalimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza,Joan John akitaja majina ya washindi katika michezo.Wa pili kutoka kulia ni Mwalimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza, John Shayo.
Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akikabidhi zawadi ya saa kwa mshindi wa mbio za mita 100 kwa kundi la vijana wa kiume.
Kijana akiangalia zawadi ya saa baada ya kukabidhiwa.
Kijana akishikana mkono na Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu wakati wa zoezi la kugawa zawadi za jumla kwa washiriki wa bonanza.
Vijana wakiendelea kupokea zawadi za chupa za maji.
Picha ya pamoja washiriki wa bonanza la michezo.
Washiriki wa bonanza la michezo wakiwa katika picha za vurugu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post