RAIS WA KOREA KASKAZINI ATUMIA TRENI KWENDA VIETNAM KUKUTANA NA RAIS TRUMP

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yumo ndani ya treni akielekea nchini Vietnam kwa ajili ya mkutano wake wa pili wa kilele na rais Donald Trump wa Marekani. 

Kim ameambatana na Kim Yong Chol, ambaye ndie mpatanishi muhimu katika mazungumzo na Marekani. Mkutano wa pili baina ya Kim na Trump umepangwa kufanyika Jumatano na Alhamis wiki ijayo mjini Hanoi. 

Mkutano wa kwanza uliofanyika nchini Singapore mwezi Juni, ulimalizika bila ya makubaliano muhimu juu ya kusistishwa miradi ya kinyukilia ya Korea Kaskazini. 

Katika mkutano huo, wataalamu wanasema Kim atajaribu kuimarisha mahusiano na Marekani pamoja pia na kuondolewa vikwazo. Safari za nje za kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kawaida hupangwa kwa siri. 

Zaidi ya siku mbili zitahitajika kwa treni anayosafria Kim kuzunguka masafa ya maelfu ya kilomita kupitia mji wa mpakani wa China-Dandong hadi Vietnam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527