Picha : AGAPE YATOA ELIMU YA MAJUKUMU YA WAJUMBE WA KAMATI ZA MTAKUWWA KATA YA DIDIA


Shirika lisilo la kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) limekutana na kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kuwapa elimu kuhusu majukumu yao katika kutekeleza mpango huo.

Elimu hiyo iliyokwenda sanjari na Mazungumzo baina vizazi yaliyokutanisha pamoja makundi ya vijana,wanawake na wazee imefanyika Februari 16,2019 katika shule ya msingi Didia kwa kukutanisha  wajumbe 216 kutoka vijiji vya kata ya Didia.

Akitoa elimu kuhusu MTAKUWWA, Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo alisema Mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wadau ili kukomesha vitendo vya kikatili katika jamii.

“Kamati zipo kwa niaba ya jamii kuisadia serikali ili kuhakikisha matukio ya ukatili dhidi ya watoto na wanawake yanatokomezwa,hivyo lazima wajumbe watambue majukumu yao”,alisema Mweyo.

Aliwataka wajumbe wa kamati za MTAKUWWA kutoa elimu kwenye mikusanyiko mbalimbali ya watu kuhusu madhara ya vitendo vya kikatili huku akiwakumbusha wazazi na walezi kuwa na urafiki na watoto wao na kuwapa elimu kuepuka kufanyiwa vitendo vya kikatili.

Naye Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na ndoa za utotoni unaotelezwa na shirika la Agape wa ufadhili wa Firelight Foundation, Mustapha Isabuda alisema Agape inashirikiana na serikali kutekeleza MTAKUWWA kwenye vijiji vitano vya kata ya Didia ambavyo ni Mwamalulu,Mwanono,Bukumbi,Didia na Chembeli.

“Leo tumekutana na wajumbe wa kamati za MTAKUWWA kutoka vijiji vya kata ya Didia ili kuwapa elimu juu ya wajibu na majukumu yao katika kutekeleza mradi huu kwani shughuli zinazofanywa na Agape zinachangia utekelezwaji wa maeneo 8 yaliyoainishwa kwenye MTAKUWWA”,alieleza.

“Pia vijana,akina mama na wazee wa wamefanya mazungumzo baina ya vizazi kwa kuchambua mila na desturi zinazopaswa kuendelezwa na zile zinazopaswa kutokomezwa katika jamii,hili ni eneo mojawapo pia kwenye maeneo 8 ya MTAKUWWA”,aliongeza.

Aidha alisema ni jukumu la wadau wote katika jamii kuhakikisha wanapiga vita mimba na ndoa za utotoni kwa kuepuka mila na desturi kandamizi.

Isabuda alikemea tabia za wanaume kunyanyasa na kutelekeza wake zao huku akiwashauri wanaume kuwashonea wake zao sare za shule ili waache kutamani wanafunzi.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Elizabeth Mweyo akitoa elimu kuhusu majukumu ya wajumbe wa kamati za Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake (MTAKUWWA) katika kata ya Didia - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Elizabeth Mweyo akiwasisitiza wajumbe wa kamati za MTAKUWWA katika vijiji vya kata ya Didia kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wajumbe wa kamati za MTAKUWWA wakimsikiliza Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Elizabeth Mweyo.
Wajumbe wa kamati za MTAKUWWA wakifuatilia mada.
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Elizabeth Mweyo akitoa mada kuhusu Ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
Wajumbe wa kamati za MTAKUWWA wakifuatilia mada.
Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na ndoa za utotoni unaotelezwa na shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwaomba wajumbe wa kamati za MTAKUWWA kuwa mstari wa mbele katika kupiga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii.
Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na ndoa za utotoni unaotelezwa na shirika la Agape, Mustapha Isabuda akizungumza wakati wa majadiliano ya makundi ya vijana,wanawake na wazee kuhusu mila na desturi zinazopaswa kuendelezwa na zile zinazopaswa kutokomezwa katika jamii. Mila na desturi ni moja ya maeneo katika MTAKUWWA.
Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na ndoa za utotoni unaotelezwa na shirika la Agape, Mustapha Isabuda akizungumza wakati wa Mazungumzo baina ya vizazi na kuitaka jamii kuachana na mila na desturi zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
Kijana Emmanuel kwa niaba ya vijana wa kiume akielezea kuhusu mila na desturi zinazopaswa kuenziwa na zile mila na desturi zisizofaa katika jamii ikiwemo kuozesha watoto wadogo.
Mashaka Daudi akiwakilisha kundi la wazee akielezea kuhusu mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo kutopeleka watoto shule,mfumo dume na wanaume kutelekeza familia na kukimbilia mjini.
Salma Hamis akiwakilisha kundi la vijana wa kike akielezea kuhusu madhara ya mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Tatu Said akiwakilisha kundi la wanawake akielezea kuhusu vitendo vya kikatili vinavyofanywa na wanaume kama vile kuuza mali za ndani na kuoa wanawake wengine huku familia ikiteseka.
Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na ndoa za utotoni unaotelezwa na shirika la Agape, Mustapha Isabuda akihamasisha jamii kuachana na mila na desturi zinazochangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake.
Afisa Mtendaji wa kata ya Didia Jackson Maganga akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu mila na desturi katika jamii ambayo ni moja ya maeneo katika MTAKUWWA.

Awali, Meneja Mradi wa Kuzuia Mimba na ndoa za utotoni unaotelezwa na shirika la Agape, Mustapha Isabuda akitoa mwongozo wa kazi ya kundi la vijana wa kike kuhusu mila na desturi.
Veridiana William akiongoza mazungumzo kwenye kundi la akina mama kuhusu mila na desturi katika jamii.
Wazee wakidajili kuhusu mila na desturi zinazopaswa kuenziwa na zile ambazo hazifai kuwepo katika jamii.
Vijana wa kiume wakiendelea na mazungumzo kuhusu mila na desturi katika jamii.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527