Picha : SBL YAWAKUTANISHA WANAWAKE KUADHIMISHA SIKU YA WAPENDANAO 'VALENTINE'S DAY'

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku ya wapendano duniani
maarufu kama ‘Valentine’s Day’ Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) imewakutanisha wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua
mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Alhamisi Februari 14, 2019 Mwenyekiti wa wanawake wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema lengo kubwa ni kuwainua wanawake ndani na nje ya ofisi kupitia jukwaa maalumu lijulikanalo ‘SBL spirited women’.

Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya
kampuni hiyo yaliyopo Chang’ombe jijini hapa pamoja na matawi yaliyopo mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro.

“Lengo ni kuwainua wanawake katika nyanja tofauti sio tu katika kazi lakini pia nje ya ofisi na kwa mwaka huu tumeona tujumuike
pamoja tuonyeshe upendo wetu kwa wanawake wote wa Serengeti na kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuendeleza kiwanda chetu,” amesema
Rwehumbiza.

Rwehumbiza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL amesema katika siku hiyo ya wapendanao kampuni ya Serengeti inawakumbusha watanzania kuzingatia unywaji
kiistaraabu ili kuepusha ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini.

“Kwa wateja wetu tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja na sisi kwa sababu uwepo wetu unategemea zaidi wafanyakazi na vilevile wanywaji wetu wakubwa,” amesema. 

Wanawake hao walionyesha umaridadi kwa kuvaa mavazi ya rangi nyekundu ambayo huvaliwa katika siku hiyo na kukabidhiwa kinywaji maalumu kijulikanacho kama ‘Baileys’ kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti.
Mwenyekiti wa wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL) Anitha Rwehumbiza akizungumza wakati
wa maadhimisho ya siku ya wapendandanao duniani (Valentine’s Day) ambapo SBL imeadhimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kupitia jukwaa liitwalo ‘SBL spirited women’ ili kujadili mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.
 
Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakionyeha Kinywaji maalumu kwaajili ya wanawake kijulikanacho kwa jina la Baileys wakati wa hafla ya kuazimisha siku ya wapendanao
‘Valentine’s Day’ iliyofanyika kwenye Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Chang’ombe jijini hapa. 
Wafanyakazi wa Sereneti Breweries tawi la Moshi wakifurahi wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendanao.
Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya maadhimisho ya
siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kujadili mchango wao katika ukuaji wa kampuni hiyo.
Wafanyakazi wanawake maarufu kama SBL spirited women kutoka mkoani Mwanza wakiwa kwenye vazi la rangi nyekundu wakati wa siku ya wapendanao 'Valentine's Day'

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527