AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUINGILIA MSAFARA WA RAIS

Adriunus Landnam (34), mkaazi wa Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingilia msafara wa Rais wa Zanzibar.

Adriunus ambae ni Mfaransa wa Swedzan House akiwa dereva wa gari yenye namba za usajili Z 724 FF private akitokea mjini kueleka shamba alipatikana akitenda kosa hilo huko Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.

Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashitaka wa serikali Asma Juma Khamis, mbele ya hakimu Rauhiya Hassan Bakari, alidai kuwa mtuhumiwa huyo alipatikana na kosa hilo siku ya Jumatano ya Febuari 20, mwaka huu mnamo majira ya saa 03:30 asubuhi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kuingilia msafara wa Rais ni kosa kinyume na kifungu 128 (2) (3) cha sheria namba 7 sheria za Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post