ORODHA YA SIMU AMBAZO HAZIKAMATI TENA WHATSAPP, NA ZINAZOKARIBIA KUFUNGIWA


Wamiliki wa simu zinazotumia programu endeshi ya simu aina ya Series 40 wamekuwa hawawezi tena kutumia mtandao wa WhatsApp kwenye simu zao.

Hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao wa kijamii wa WhatsApp wa kuacha kutengeneza app yake kwa njia ambayo inaweza kutumiwa katika simu hizo.

Wengi zaidi wataathirika katika kipindi cha mwaka ujao, 1 Februari, 2020 ambapo simu nyingi zikiwemo baadhi ya iPhone zitapoteza uwezo wa kutumia WhatsApp.

Hata kabla ya wakati huo kufika, Facebook wameonya kwamba "kwa sababu hatutakuwa tukitengeneza na kuboresha app yetu tukizizingatia, huenda baadhi ya uwezo wake ukaathirika wakati wowote."

Zitakazoathirika mwaka ujao ni za Android zinazotumia Android 2.3.7 na miundo ya awali, pamoja na iPhone zinazotumia iPhone iOS 7 kwenda nyuma. Kwa sasa, mfumo wa Android umefikia 9.0. [Unaweza kuangalia mfumo unaotumiwa na simu yako kwenye 'Settings', kisha sehemu ya 'Software/Software Info]

Wanaotumia Android 2.3.7 kwenda nyuma hawawezi kufungua akaunti mpya za WhatsApp.

Ndipo uweze kutumia mtandao huo kwa sasa unahitajika kuwa unatumia Android 2.3.3 kwenda juu na Windows Phone 8.1 kwenda juu.

Kwa sasa, walioathirika zaidi ni wanaotumia baadhi ya simu za Nokia zinazotumia mfumo endeshi wa Series 40 ambao wakati mwingine huitwa S40 OS. Miongoni mwa simu maarufu zilizoathirika ni Nokia 6300.

Simu ya mwisho kutengenezwa ambayo ilikuwa inatumia S40 ilikuwa Nokia 515 ambayo ilizinduliwa mwaka 2013.

Ingawa baadhi ya simu hizi ni za bei nafuu na hutumiwa na watu wa kipato cha wastani au cha chini, kuna wanaotumia simu aina ya pia simu za Vertu Signature S ambazo zilikuwa ghali sana na ambazo hutumia programu hiyo endeshi pia.

Wakati wa kuanza kuuzwa kwa simu hizo zilikuwa zinauzwa takriban £8000 (Tshs23m; Kshs1m), ingawa hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita na huenda wengi wao wamenunua simu nyingine au wana uwezo wa kununua simu nyingine kwa urahisi.

Simu zilizoathirika kwa sasa

  • Nokia 206 Single SIM na dual SIM
  • Nokia 208
  • Nokia 301 Single SIM na dual SIM Chat Edition
  • Nokia 515 zinazouzwa zikiwa na WhatsApp
  • Nokia Asha 201
  • Nokia Asha 205 Chat Edition
  • Nokia Asha 210
  • Nokia Asha 230 Single SIM na dual SIM
  • Nokia Asha 300, 302, 303, 305, 306, 308, 309, 310, 311
  • Nokia Asha 500, 501, 502, 503
  • Nokia C3-00
  • Nokia C3-01
  • Nokia X2-00
  • Nokia X2-01
  • Nokia X3-02
  • Nokia X3-02.5
Simu ambazo haziwezi kutumia WhatsApp na tarehe ya kuacha kutumia
  • Nokia Symbian S60 baada ya Juni 30, 2017
  • BlackBerry OS na BlackBerry 10 baada ya Desemba 31, 2017
  • Windows Phone 8.0 na miundo ya awali Desemba 31, 2017
  • Nokia S40 baada ya Desemba 31, 2018
  • Android 2.3.7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
  • iPhone iOS 7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020

Simu nyingine zisizotumia WhatsApp

Kufikia Juni mwaka 2017, huduma ya WhatsApp pia ilikuwa imeacha kutumika tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zilizotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema wakati huo kwamba inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."


Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.

Simu zilizotumia Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6 hata hivyo zilifungiwa mwishoni mwa 2016.

Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka 2016.

Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani

Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawawezi kutumia WhatsApp:

  • Android 2.1 na Android 2.2
  • Windows Phone 7
  • iPhone 3GS/iOS 6
  • BlackBerry OS and BlackBerry 10
  • Nokia S40
  • Nokia Symbian S60



Wanaotumia simu zilizofungiwa wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.Simu ya Blackberry

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527