HATIMAYE TFF YAMREJESHA MWENYEKITI WA YANGA


Makao makuu ya klabu ya Yanga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa kamati yake ya Rufaa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake, Kenneth Mwenda, imemrejesha mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yono Kevela ambaye alikuwa ameenguliwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kusikiliza rufaa aliyokata mgombea huyo akilalamikia maamuzi ya kuenguliwa jina lake kwenye majina ya wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, kwa madai kuwa aliomba nafasi mbili, nyingine ya Uenyekiti.

Kevela sasa anaungana na Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wakati wagombea Uenyekiti ni Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga.

Wagombea 16 wa nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.

Viongozi waliojiuzulu ni aliyekuwa Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wanne, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah hivyo nafasi zao zitazibwa katika uchaguzi huo wa Januari 13, 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post