MWANAMKE AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA MAMBA

Mwanamke mmoja raia wa Indonesia ameuawa na Mamba huko Sulawesi baada ya kuanguka karibu nae.


Deasy Tuwo, 44, inasemekana alikuwa akimlisha Mamba huyo kwenye shamba huko Sulawesi mahali anapofanyia kazi na sehemu ambayo mamba huyo alihifadhiwa bila kibali.


Mamba huyo mwenye kilo 700 aitwae Merry inasemekana alimng'ata mkono na sehemu kubwa ya tumbo.

Mnyama huyo amehamishiwa katika hifadhi wakati mamlaka ikimtafuta mmiliki, Tuwo alivamiwa na mamba wakati akimpatia chakula.

Bi Tuwo alikuwa ni msimamizi wa maabara katika eneo hilo na alikuwa akimpatia chakula Merry tarehe 10 mwezi januari ambapo aliangukia mikononi mwamnyama huyo.

Wafanyakazi wenzie waliuona mwili wake asubuhi ya siku inayo fuata.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527