ASKARI SABA WA " DHAHABU MWANZA" WASIMAMISHWA KAZI KWA KUOMBA RUSHWA

Jeshi la Polisi Tanzania  tarehe 11/01/2019, limewasimamisha kazi askari saba (7) wa vyeo mbalimbali kwa kutenda kosa kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi na tayari wamefikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayo wakabili.

Hatua hii imechukuliwa, baada ya askari hao kuomba rushwa ya bilioni moja na baadae kupokea rushwa ya milioni mia saba toka kwa mfanyabiashara wa dhahabu aitwaye Sajid Abdalah Hassan ambaye walimkamata akiwa na dhahabu kiasi cha kilogramu 319.59, yenye thamani ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.

Askari hao waliosimamishwa kazi ni;
  1.     E.4948 CPL Dani Isack Kasala
  2.     F.1331 CPL Matete Maiga Misana
  3.     G.1876 PC Japhet Emmanuel Lukiko
  4.     G.5080 PC Maingu Baithaman Sorrah
  5.     G.6885 PC Alex Elias Nkali
  6.     G.7244 PC Timoth Nzumbi Paul
  7.     H.4060 PC David Kadama Ngelela.
Aidha, kuhusu Afisa SSP: Moris Okinda ambaye alikuwa kiongozi wa askari hao walioomba na kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha, mamlaka yake ya kinidhamu tayari imemsimamisha kazi na tayari amefikishwa mahakamani pamoja na askari hao.

Pamoja na askari hao, pia wamefikishwa mahakamani watuhumiwa wengine wa nne waliokamatwa huko Kigongo feri Wilayani Misungwi wakitorosha madini hayo ya dhahabu kutoka Tanzania kwenda Nchi jirani ya Rwanda.

Watuhumiwa waliokamatwa wakitorosha madini hayo ya dhahabu ni;
  1. Sajid Abadalah Hassan, miaka 28, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa Ilala Dar es Salaam na Mwanza mtaa wa pamba ‘A’.
  2. Kisabo Kija @ Mkinda , miaka 55, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa mwatulole –Geita
  3. Emmanuel Ntemi, miaka 63, dereva, mkazi wa kijiji cha mwatulole –Geita
  4. Hassan Sadiq Hassan, miaka 28, Mhindi, Raia wa Pakistani, mkazi wa Mwanza mtaa wa Pamba ‘A’, Mfanyakazi wa duka la kuuza vito.
Kufuatia sakata hili, Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tunaendelea na uchunguzi wa kina ili tuweze kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hili.

Imetolewa na;
CP: Robert Boaz
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania
11 January, 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527