CLIFORD NDIMBO KAULA CAFCliford Mario Ndimbo.

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF), limemteua Afisa Habari wa TFF kuwa Afisa Habari wa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka nchini (TFF), Ndimbo atasimamia taarifa zote za mchezo huo utakaopigwa Ijumaa Februari 1, 2019 nchini Afrika Kusini kwenye uwanja wa Loftus Versfeld.

Mamelodi Sundowns na ASEC Mimosas zipo kundi A na mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwa kila timu katika hatua hiyo ya makundi.

Timu hizo zote zina alama 3 baada ya kushinda mchezo mmoja na kufungwa moja. Mamelodi wapo nafasi ya tatu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa huku ASEC wakiwa katika nafasi ya 3.

Vinara wa kundi hilo ni timu ya Wydad Casablanca ambayo nayo ina alama 3 huku Lobi Stars ya Nigeria ikiwa na alama 3 katika nafasi ya 4 ya kundi hilo.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527