ONYO LA RAIS MAGUFULI KWA ALIOWATEUA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutotumia mamlaka yao vibaya kwa kuwaweka ndani baadhi ya watendaji wenzao ikiwa ni kinyume na sheria.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya mbili, Mwanga pamoja na Tarime ambapo alibainisha sababu za kuwatengua waliokuwa kwenye nafasi hizo kuwa ni kutokana na kutumia vibaya mamlaka yao.

 "Mnasheria na mamlaka mlizopewa msizitumie vibaya sheria mnazo lakini msizitumie vibaya mtu anawekwa ndani halafu hamumpeleki mahakamani", alisema 
Rais Magufuli.

"Viongozi wengi wamelizungumzia hili namimi nalirudia, kuna masuala mengine hayahitaji mtu kuweka ndani yanahitaji kutoa maelekezo tu", aliongeza Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amehoji juu ya hatua mtu anayetuhumiwa kubaka watoto 11 kushindwa kukutwa na hatia na mahakama baada ya ushahidi kutojitosheleza.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527