MAREKANI YAISHITAKI KAMPUNI YA HUAWEI KWA TUHUMA YA WIZI

Marekani imewasilisha kesi 23 dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei.

Marekani imeishtaki kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei na afisaa mkuu wake wa fedha, Meng Wanzhou.

Mashataka hayo ni pamoja na ubadhirifu wa fedha, kupinga utekelezaji wa haki na wizi wa teknolojia.

Kesi hiyo huenda ikazua mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China hali ambayo itaathiri biashara ya kampuni hiyo.

Kampuni ya Huawei imekanusha madai hayo.

Katika taarifa, Huawei imesema kuwa imeghadhabishwa na mashtaka dhidi ya yake.

Imesema kuwa haikufanya makosa yote yanayodaiwa ilitekeleza na kwamba haina ufahamu wa kosa alilotekeleza Bi Meng.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post