TAZAMA JINSI DIAMOND ALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE KENYA


Wasanii watakaofanya show leo Jumatano  katika Tamasha la Wasafi Festival nchini Kenya kutoka Tanzania wamepokewa kwa shangwe kubwa na Wakenya hapo jana.

Awali show hiyo iliingiwa na sitofahamu baada ya msanii Diamond na Rayvanny kutoruhusiwa kufanya onesho nje ya nchi baada ya kufungiwa na BASATA kwa kosa la kuimba wimbo Mwanza ambao ulifungiwa na baraza hilo.

Lakini juzi baraza hilo lilitoa ruhusa kwa waimbaji hao ya kufanya onesho kwa madai adhabu ya kufungiwa ilikuja kwa wawili hao wakati tayari wameshaingia makubaliano ya onesho la Kenya.

Baada ya team hiyo kuwasili nchini Kenya, Rais wa WCB Diamond Platnumz aliwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwaajili ya onesho hilo la aina yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527