WAANDISHI WA HABARI WAKUMBUSHWA KULINDA MAADILI HABARI ZA AFYA

Waandishi wa habari nchini wamekumbushwa kulinda maadili na matumizi ya takwimu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hasa katika uandishi wa habari za afya. 

Mwezeshaji wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma za Tohara kinga kwa wanaume yanayoendelea mkoani Geita, Temigunga Mahondo amewakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa kutumia takwimu katika uandishi,ukweli na usahihi kwa kufanya utafiti,kujiridhisha na kulinda utu na haki ya faragha. 

“Mwandishi wa habari anapoandika habari ambayo pengine inamashaka inapunguza uaminifu na kushusha heshima ya chombo husika,hivyo mwandishi wa habari anatakiwa kujiridhisha kwenye mamlaka husika lakini pia kwa kufanya utafiti binafsi ili kupata ukweli na usahihi wa habari unayoiandika kwa walaji” ,amesema Mahondo. 

Ikiwa leo ni siku ya pili ya mafunzo hayo,washiriki wameunda makundi matatu ambayo yanatarajia kuandaa makala fupi katika Radio,Luninga na Gazeti, makala yatakayoangazia masuala ya afya ya uzazi ikiwa ni pamoja Tohara kinga kwa wanaume kwa kuzitazama faida na madhara yake. 

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Shirika la IntraHealth International Inc. kwa waandishi wa habari kutoka Mkoa wa Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Kagera na Kigoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa utoaji wa huduma za tohara kwa wanaume ambayo ni afua mojawapo ya kuzuia maambukizi ya VVU.

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO SIKU YA PILI YA MAFUNZO

Mwezeshaji wa mafunzo ya huduma ya tohara kinga kwa wanaume Temigunga Mahondo akitoa darasa na ufafanuzi wa kina kuhusu umuhimu wa tohara kinga kwa wanaume.
Mwandishi wa habari wa Radio SAUT Mwanza Rose Nicholaus akiwasilisha habari iliyoandikwa na kikundi namba moja ambacho kiliandika habari kuhusu idadi na asilimia ya wanaume ambao wamefanyiwa tohara kinga mkoa wa Geita.

Mwandishi wa habari wa Clouds media Mkoa wa Shinyanga Kasisi Kosta akiwasilisha habari ya kikundi cha pili ambacho kimeandika habari kuhusu shughuli za kiuchumi zinavyokwamisha Tohara kwa wanaume mkoa wa Geita.

Afisa habari mkoa Geita Boaz Mazigo akiwasilisha kazi ya kikundi namba tatu kuhusu ongezeko la maambukizi ya virusi vya UKIMWI akishabiisha na wanaume kutoitikia mwito wa kujitokeza kufanyiwa tohara,ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI na magonjwa ya zinaa,na kutoa wito kwa jamii kujitokeza na kuhamasisha wanaume kufanyiwa tohara kinga.

Afisa kutoka shirika lisilo la kiserikali la IntraHealth International Inc.kitengo cha habari na mawasiliano Mary Mndeme akihariri habari za vikundi vitatu vilivyowasilisha habari zao na hapa kikundi namba mbili kikaibuka kinara kwenye uandishi uliosheheni vigezo vya uandishi,na kuwakumbusha waandishi kufanya uhakiki wa kazi kabla ya kuzituma mahali husika kwa ajili ya walaji(wasikilizaji,watazamaji na wasomaji).

Mafunzo yakiendelea ukumbini.

Kikundi namba moja wakijadili ni kwa namna gani waandishi wa habari wanaweza kutoa mchango kubadili mitazamo hasi ya jamii kuhusu huduma za tohara kinga.

Kikundi namba tatu wakijadiliana namna ya kuishawishi na kuielimisha jamiii kuhusu umuhimu wa Tohara kinga.

Kikundi namba tatu kikijadili wazo la habari kuhusu mila na desturi zinavyokwamisha zoezi la tohara kwa wanaume Mkoa wa Geita.

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye makundi yao wakijadili mawazo ya kutengeneza habari ambazo zitakuwa na matokeo ya manufaa kwa muda mfupi na mrefu. 


Picha zote na Malaki Philipo Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527