ALIKIBA KUACHIA NGOMA MPYA SHOW YA 'FUNGA MWAKA NA KING KIBA' | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, December 12, 2018

ALIKIBA KUACHIA NGOMA MPYA SHOW YA 'FUNGA MWAKA NA KING KIBA'

  Malunde       Wednesday, December 12, 2018
Msanii wa muziki wa kizazi Ally Salehe Kiba a.k.a Alikiba ameweka wazi kuwa December 19 mwaka huu ataachia nyimbo zake mbili.

Hiyo ni katika show yake kubwa ya kufunga mwaka, huku show yake na muimbaji maarufu Afrika, Yvonne Chaka Chaka kutokea Afrika Kusini ikihairishwa hadi February 2019. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Kuelekea kwenye show yangu kubwa ya mwaka 'Funga Mwaka Na King Kiba' December 19, 2018 pale Next Door Arena, nitaachia “HITS” zangu mbili kabla mwaka haujaisha pamoja na kuzindua rasmi kinywaji changu cha Mofaya Energy Drink.

"Sema kuna mabadiliko ya tarehe ya show yangu na Mama Yvonne Chaka Chaka pamoja na King Of Best Melodies, Christian Bella christian kutoka December to February 2019, the month of Love ❤"

Kwa sasa Alikiba anafanya vizuri na wimbo unaokwenda kwa jina la Mwambie Sina alioshirikiana na kundi lake la Kings Music ambalo pia kwa sasa linafanya vizuri na wimbo uitwao, Toto.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post