TAHA/STANBIC BANK WAANDAA MAONYESHO YA TAASISI ZA KIFEDHA ARUSHA


Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya wakulima nchi za SADEC Dkt Sinare Yusuph Sinare 
Mwenyekiti wa (TAHA) Erick Ngimario akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo
Meneja wa Fredrick Max Meneja wa Bank ya Arusha Stanbic Bank akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Taasisi za Kifedha Jijini Arusha leo

Na. Vero Ignatus, Arusha

Wito umetolewa Taasisi za kifedha kuna kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwani kuna fursa kubwa haswa kilimo cha mbogamboga

Hayo yamesemwa na Dkt Sanare Yusuph Sanare katika maonyesho za Taasisi ya Kifedha kuhusu fursa za mitaji kwenye kilimo yameliyozinduliwa leo Jijini Arusha.

Kauli mbiu uhakika wa mitaji ili kukuza kilimo. Biashara kuelekea kuelekea uchumi wa viwanda.

Mgeni rasmi katika maonyesho Dkt Sanare amesema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuwaunganisha watoa huduma za kifedha na wakulima haswa wa mbogamboga(hot culture).

Dkt Sanare amesema tatizo kubwa la mkulima ni mtaji ambapo benki za biashara nyingi zilikuwa hazitoi mkopo kwenye sekta ya kilimo lakini hivi sasa kumeanza kuwa na mabadiliko makubwa wameanza kuona umuhimu wa kutoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAHA Erick Ngimario amesema kuwa Tanzaniabya Viwanda ambayo watu wote wanaiwania msingi wake mkubwa ni kilimo ambapo tasnia ya kilimo cha mbogamboga ni sehemu kubwa sana.

Amesema Tanzania inakwenda vizuri na kilimo cha mbogamboga kwani kuna ardhi nzuri yenye rutuba, maji kwa kiasi kikubwa, maziwa na mito na sehemu zote ambazo zinauwezekano wa kulima mboga, viungo na matunda ambapo ni sehemu kubwa ya kilimo hapa nchini.

''TAHA inaamini kuwa kilimo hichi cha hotculture ni kilimo cha biashara ni kilimo ambacho kina faida na hasara na kila anayeingia humo anaangalia faida", alisema.

Amesema kutokana na hayo lazima mkulima apate fursa ya kukopa ili aweze ili aweze kuendesha kilimo na apate faida kwani taasisi ambazo zimeweka maonyesho zinamuwezesha mkulima kukopa, kufanya kazi na kulipa.

'' Hakuna tasnia ambayo ni rahisi sana kulipa kama tasnia ya kilimo cha mbogamboga kwani haitegemei sana mvua, na mambi ambayo hayana usimamizi maana kinategemea umwagiliaji''.

Amesema kilimo hicho hutegemea sana mpangilio ulime wakati upi na vilevile kuvuna uvune wakati upi kwani masoko nayo ni mihimu.

Aidha amesisitiza kuwa maonyesho hayo siyo ya mara ya kwanza kwani kumeshakuwa na maonyesho Kama hayo mara nyingi na wengi wawanachama wao wameitumia fursa hiyo na wamefanikiwa.

Amesema TAHA siku zote imekuwa ni kuingo kati ya wakulima na masoko, kati ya wakulima na serikali na Taasisi za serikali na katika ugani ambapo wakulima wanapata ushauri wa kilimo, ushauri wa masoko, na wanatumia mitandao kufanya hivyo.

''Kwa jumla wanachama wetu ambao mtandao wetu ambao umeenea karibia nchi nzima wanategemea mambo mengi kutoka TAHA'',alisema Ngimario.

Kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa wa mitaji na wakulima mwenyewe kwa wenyewe inakuwa vigumu kufanya hivyo.

Amesema STANBIC BANK Fredrick Max mwaka huu 2018 wameanzisha dawati la Kilimo litakuwa linaangalia mazingira yote ya kilimo nchini Tanzania.

Amesema kuwa Banki hiyo inakijitahidi kufanya kazi na washirika kama TAHA, PASS, wakulima na wafanyabiashara wa kilimo kwa ujumla.

Maonyesho hayo yameshirikisha mabenki mbalimbali sambamba na watoa huduma nyingine ikiwemo TRA na RITA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post