DAR KUONGOZWA NA CCM,UKAWA

Na Christina Mwagala
UCHAGUZI wa Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam, umefanyika leo ambapo wajumbe wa Baraza hilo wamekubaliana kwa kauli moja kuwa na Manaibu wawili kutoka Chama Cha Wananchi CUF na mwingine Chama Cha Chamapinduzi CCM.

Hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa idadi sawa ya wajumbe kwa pande zote mbili ambapo Ukawa ulikuwa na wajumbe 12 huku CCM ikiwa na wajumbe 12.

Akizungumza wakati wakutangaza uamuzi huo ulioafikiwa na wajumbe wa Baraza hilo, Mstahiki Meya Isaya Mwita alisema kuwa kutokana na hali hiyo kila mmoja ataongoza kwa kipindi cha miezi mitatu hadi Juni 30 mwaka 2019.

Meya Mwita alieleza wajumbe wa baraza hilo kuwa, wamefikia uamuzi huo kwani viongozi wamechaguliwa kwa ajili ya kuleta maendeleo ya waanchi bila kujali vyama vyao.

Alisema kuwepo kwa viongozi wa vyama viwili tofauti haita wakosesha wananchi maendeleo kwakuwa wote wamechaguliwa kwa lengo la kuwatumikia wakazi wa jinnini hapa.

Meya Mwita alitumia nafai hiyo kuwasihi manaibu hao walioteuliwa kuonyesha ushirikiano mkubwa kwa ajili ya kuleta maendeleo jijini hapa kwakuweka itikadi ya vyama vyao pembeni.

“ Ndani ya ofisi hii kupata wasaidi kutoka vyama tofauti sio dhambi, lengo langu ni kulifikisha jiji sehemu ambayo inatakiwa, ninaimani kuwa walioteuliwa leo tutasaidiana bila kujali itikadi za vyama vyetu” alisema Meya Mwita.

Kabla ya kufanyika kwa maamuzi hayo, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sita alitoa hoja baada ya kuwepo kwa mvutano mkali kuwa baraza lijigeuze kamati ilikufanya maamuzi ambayo yatakuwa na maslahi kwa wananchi kuliko kuendelea na mabishano.

“ Ndugu mwenyekiti hakuna haja ya kuendelea kubishana ,wote hapa tunafanya kazi kwa ajili ya wanachi wa jijini hapa,ningeshauri tujigeuze kamati ili kufikia muafa wa jambo hili.

Baada ya hoja hiyo kutolewa,wajumbe wa baraza hilo walikubaliana kuwa kamati ,ambapo baada ya nusu saa,walirudi kuwa baraza na hivyo Meya Mwita kutoa maamuzi ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo umefanyika leo ikiwa ni baada ya aliyekuwa Naibu Meya Mussa Kafana kujiuzulu nafasi yake na kujiunga na CCM Septemba mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527