MTOTO SHABIKI WA MESSI ATOROKA NYUMBANI


Murtaza Ahmadi akiwa na Lionel Messi

Mtoto Murtaza Ahmadi raia wa Afghanistan ambaye alijipatia umaarufu duniani kote kutokana na ushabiki wake kwa nyota wa Barcelona Lionel Messi, ametoroka nyumbani kutokana na vitisho vya kundi la Taliban.

Imeripotiwa kuwa Murtaza amekuwa akitishiwa na kundi hilo wakidai kuwa ana pesa nyingi ambazo amepewa na Lionel Messi hivyo wanazitaka.

Mama wa Murtaza, Shafiqa, amekiri kuwa anapigiwa simu na watu wakitaka awaambie zilipo pesa ambazo mtoto huyo alipewa kama zawadi na nyota huyo wa Argentina walipokutana.

''Umekuwa tajiri, tupatie pesa ulizopokea kutoka kwa Messi la sivyo tutamteka mtoto wako" ni maneno ambayo amekuwa akiambiwa mama yake Murtaza kutoka kwa kundi lenye itikadi kali la Taliban.

Mwaka 2006 Murtaza Ahmadi mwenye miaka 7, alijizolea umaarufu mitandaoni baada ya kupigwa picha akiwa amevaa mfuko wenye mistari inayofanana na jezi ya timu ya taifa ya Argentina huku akiwa ameandika jina la Messi mgongoni.

Murtaza alipewa mwaliko wa kukutana na Messi mwaka huo ambapo walikutana nchini Qatar na mtoto huyo alifurahi kiasi cha kumganda Messi muda wote. Ilielezwa Messi alimpa zawadi mbalimbali mtoto hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post