MWIGULU NCHEMBA AACHANA NA YANGA...AJIUNGA SIMBA KUISHUGHULIKIA NKANA RED DEVILS

Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni shabiki mkubwa wa klabu ya Yanga, Mwigulu Nchemba ameweka wazi kuwa leo anaiunga mkono klabu ya Simba na atakuwa uwanjani kuipa nguvu timu dhidi ya Nkana Red Devils.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mwigulu amesema Simba inawakilisha taifa hivyo ni lazima kuiunga mkono ili iweze kutufanya vizuri.
''Hii ni Simba, hii ni Tanzania, tukutane taifa kwa Mkapa, tuwaunge mkono Simba, Vivaa Simba '', ameandika Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani.
Mbali na kuwa shabiki wa Yanga lakini kwasasa ni Rais wa klabu ya Singida United ambayo inashiriki ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa katika msimu wake wa pili tangu irejee ligi kuu.
Simba leo inashuka dimbani kuanzia saa 10:00 jioni kukipiga na Nkana Red Devils kwenye mchezo wa marudiano raundi ya kwanza. 
Katika mchezo wa kwanza uliopiga mjini Kitwe Zambia Simba ilikubali kichapo cha bao 1-0 hivyo leo inahitaji ushindi wa bao 1-0 au zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post