BENKI YA KCB YAENDESHA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA



Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB, Lightness May akizungumza kwenye kwenye semina kwa wadogo na wa kati waliokutanishwa na benki hiyo kupitia KCB Biashara Club. Semina hiyo ilifanyika Novemba 29, 2018 Gold Crest Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 lengo likiwa ni kuwapa mafunzo kuhusu muhusu usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara pamoja na sheria za kodi.
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara wadogo na wa kati (SME) Benki ya KCB, Abdul Juma akizungumza na wafanyabiashara wa Jijini Mwanza kupitia Klabu ya Wafanyabiashara (KCB Busness Club) Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakijitambulisha kabla ya kuanza kwa semina ya "KCB Club Workshop" Jijini Mwanza.
Washiriki wa semina hiyo iliyoandaliwa na Benki ya KCB Jijini Mwanza.
Hii ni semina ya pili kuandaliwa na benki ya KCB kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) baada ya semina kama hiyo kufanyika Jijini Dar es salaam mwanzoni mwa mwaka huu ambapo "KCB Busness Club" ilizinduliwa mwaka jana.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Benki ya KCBTanzania imetoa semina kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) zaidi ya200 Jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya usimamizi
wa fedha, uendeshaji wa biashara pamoja na sheria za kodi.

Semina hiyo ilifanyika Novemba 29, 2018 kupitia Klabu ya Wafanyabiashara KCB (KCB Busness Club) Jijini Mwanza, ambapo wafanyabiashara waliojiunga na klabu hiyo wanapata fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo/ semina pamoja na kupanua wigo wa biashara zao ndani na nje ya
nchi.

Akizungumza kwenye semina hiyo, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Mwanza, Emmanuel Mzava alisema benki hiyo itaendelea kutoa semina/ mafunzo mbalimbali kwa wateja wakeili kuwasaidia kukuza biashara zao hivyo wategemee semina zaidi hapo baadae.

Akiwasilisha mada kwenye semina hiyo, Sweetbert Thomas ambaye ni Mtaalamu wa Kodi aliwahimiza wajasiriamali na wafanyabishara hao kutambua umuhimu wa mifumo ya
kodi nchini inavyoguza biashara zao hatua itakayosaidia biashara zao kuendelea kukua.

Nao baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Kitana Chacha Mnanka ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Mkombozi inayojishughulisha na usafirishaji wa abiria/ mizigo majini na nchikavu mkoani Mwanza, waliishukuru Benki ya KCB kwa kuwapatia semina hiyo nakueleza kwamba itawasaidia kukuza biashara zao ambapo pia walitoa rai kwa
wafanyabiashara wengine kujiunga na Benki hiyo ili kunufaika na huduma zake ikiwemo elimu kupitia semina mbalimbali.

Nchini Tanzania, Benki ya KCB ina matawi 14 huku pia huduma zake zikipatikana katika nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini pamoja na
Ethiopia ambapo ina matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962 pamoja namawakala zaidi ya 15,000 katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ikisifika kwa
utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527