BALOZI WA TANZANIA ATOA YA MOYONI KUHUSU SIMBA


Ni ngumu kwa viongozi wa serikali kuweka wazi mapenzi yao kwa klabu za soka hususani zenye wafuasi wengi kama Simba na Yanga lakini Balozi wa Tanzania nchini eSwatini, Joseph Ndalawa amesema yeye ni shabiki mkubwa wa Simba.

Balozi huyo wa heshima, aliweka wazi hilo kwenye chakula cha usiku na wachezaji pamoja na uongozi mzima wa Simba ulioko eSwatini ambako walicheza na Mbabane Swallos na kushinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa Afrika.

''Mimi ni mpenzi mkubwa wa Simba na ninafuatilia sana tunapokuwa kwenye michuano ya kimataifa, tuliwahi kushinda goli 5 ila niwapongeze sana sasa mmeshinda 8, ongezeni bidii zaidi ili timu ifike mbali'', alisema.

Baada ya ushindi wa jumla ya mabao 8-1 Simba SC sasa itakutana na Nkana FC ya Zambia katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nkana FC yenyewe imeitoa UD Songo ya Msumbiji kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-1 baada ya kushinda mabao 2-1 ugenini kisha 1-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani mjini Kitwe, Zambia.

Mabingwa hao wa Zambia ndio timu ambayo anachezea beki wa kulia wa zamani wa Simba na Yanga, Hassan Ramadhani Kessy ambaye alianzia soka lake kwenye klabu ya Mtibwa Sugar ambayo pia inaiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post