Picha : RAFIKI SDO YAPIGA HODI MARA...YAFANYA SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA 2018 DC NYAMUBI AKIPONGEZA


Mkuu wa wilaya ya Butiama mkoani Mara, Mheshimiwa Annarose Nyamubi akionesha cheti alichopewa na Shirika la Rafiki SDO kutokana na mchango wake kwa shirika la Rafiki.

Shirika la Rafiki Social Development Organization lenye makao makuu yake mkoani Shinyanga limekamilisha ziara yake katika mkoa wa Mara kwa kufanya sherehe ya siku ya familia 'Rafiki family day' mkoani Mara ikiwa ni kilele cha ziara ya wafanyakazi wa shirika hilo iliyoanza Disemba 20,2018.

Sherehe hiyo imefanyika Ijumaa Disemba 21, 2018 katika ukumbi wa Le-Gland Beach Musoma ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Butiama Mheshimiwa Annarose Nyamubi.

Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Nyamubi alilipongeza shirika la Rafiki SDO kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuyafikia maeneo ya pembezoni. 

‘Niwapongeze sana kwa juhudi zenu na uzalendo wenu, mnafanya kazi inayoonekana na mnaenda kwenye maeneo yale magumu zaidi, lakini niwaombe muutazame sana mkoa wa Mara maana vitendo vya ukatili vimekithiri",alisema Nyamubi. 

"Nyinyi Rafiki SDO ni mfano wa kuigwa sio kama mashirika mengine mpaka unatamani yafutwe maana hayaifikii jamii bali wanajinufaisha wachache kwa mgongo wa jamii’,aliongeza Nyamubi.

Naye,Mkurungezi Mtendaji wa shirika la Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali katika jitihada za kuikomboa jamii katika janga la ukatili wa kijinsia, kwa kuendelea kutoa elimu huku akiweka bayana kuwa mwaka 2019 wataanza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii mkoani Mara ukiwemo ule wa kupinga vitendo vya ukatili na manyanyaso. 

"Tumefanya sherehe hii kwa ajili ya kupongezana na kujitathmini kazi tulizofanya kwa mwaka 2018, lakini pia kuwa karibu zaidi na ninyi wadau wetu, katika kuongeza nguvu ya mapambano haya tutaendelea kushirikiana na watalamu waliopo katika halmashari zote na wakuu wote wa wilaya na viongozi wengine wa serikali",alisema Ng’ong’a. 

Mwenyekiti wa bodi ya Rafiki SDO, Ghatti Magana aliwataka wafanyakazi kuendeleza mshikamano wao na kuwa na nidhamu katika kazi kwani kwa kufanya hivyo itawaongezea nguvu ya ushirikiano hivyo kuifikia jamii na kuiletea maendeleo.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Butiama Mheshimiwa Annarose Nyamubi akizungumza wakati wa sherehe ya Familia ya Rafiki 'Rafiki family Day' iliyofanyika usiku wa Disemba 21,2018 ambapo aliwataka wafanyakazi wa Rafiki kufanya kazi kwa weledi zaidi na pia kuwekeza nguvu katika kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Mara kwani umekithiri kwa vitendo vya ukatili.
Mkuu wa wilaya ya Butiama,Mh. Annarose Nyamubi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki SDO Gelard Ng'ong'a.
Wanafamilia wa Rafiki SDO wakipata vinywaji.
Wanafamilia wa Rafiki SDO wakizungumza na Mh. Annarose Nyamubi.
Wafanyakazi wa Rafiki SDO wakiongozwa na Lydia Kashindye (kulia) kuieleta keki na Shampaigne ukumbini.
Burudani ikiendelea. 
Mjumbe wa bodi ya Rafiki SDO Seif Mande akifungua Shampaigne.
Mh. Nyamubi akipokea kinywaji.
Mkuu wa wilaya ya Butiama,Mh. Annarose Nyamubi akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng'ong'a.
Furaha na shangwe zikiendelea.
Mh.Nyamubi na familia ya Rafiki SDO wakichukua chakula.
Zoezi la kuchukua chakula likiendelea.
Wanafamilia ya Rafiki SDO wakifurahia zawadi zilizotolewa na shirika ambapo kila mmoja alipewa zawadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng'ong'a akiwa amebeba zawadi yake.
Mfanyakazi wa Rafiki SDO Tangi Clement (kulia)akipokea zawadi.
Zoezi la utoaji zawadi likiendelea.
Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng'ong'a na mfanyakazi wake Mariam wakikabidhiana zawadi kwa style ya kucheza muziki.
Burudani inaendelea...Mh. Nyamubi akicheza muziki na wafanyakazi wa Rafiki SDO. 
Burudani inaendelea.
Awali mchana Disemba 21,2018 : Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Musoma Gideon Obel akiwakumbusha wafanyakazi wa Rafiki SDO kushirikiana na wazee na serikali na wadau wengine katika kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa bodi ya Rafiki SDO,Ghatti Magana akitoa neno mbele ya wafanyakazi na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.
Wafanyakazi wa Rafiki SDO wakiwa katika kikao maalumu kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng'ong'a akiokota karatasi ambalo limeandaliwa katika moja ya mchezo ambapo ukiokota karatasi hiyo utakuta jina la mfanyakazi mwenzako inatakiwa ukamnunulie zawadi. 
Wanafamilia wa Rafiki SDO wakila chakula cha pamoja. 
Wafanyakazi na familia ya Rafiki SDO wakipiga picha katika ufukwe wa Ziwa Victoria.
Mjumbe wa bodi ya Rafiki SDO Seif Mande (kushoto) akiteta jambo na mkurugenzi mtendaji wa rafiki SDO kando ya ufukwe wa Ziwa Victoria.
Wafanyakazi wa Rafiki SDO wakipiga picha ya kumbukumbu katika ufukwe wa Ziwa Victoria.



Mfanyakazi wa Rafiki SDO  Lydia Kashindye akipiga picha ya kumbukumbu katika bango la Rafiki SDO mkoani Mara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527