Picha: WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RAFIKI SDO WAFANYA ZIARA KATIKA MAKUMBUSHO YA MWALIMU J.K NYERERE

Shirika lisilo la kiserikali la Rafiki Social Development Organization -SDO linalojihusisha na miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupinga ukatili wa kijinsia, limefanya ziara mkoani Mara kutembelea makumbusho ya Mwitongo wilayani Butiama alipozikwa muasisi wa taifa la Tanzania hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,iliyofanyika Desemba 20,2018, Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Rafiki SDO Gelard Ng’ong’a ameiomba jamii kujenga utaratibu wa kutembelea makumbusho hayo ili waweze kujifunza historia ya Baba wa taifa kwa kuangalia mifano halisi inayopatikana katika makumbusho hayo . 

‘Tujifunze historia ya Mwalimu Nyerere na kuna mambo mazuri aliyafanya na sisi pia tutumie nafasi hiyo kuishi kama mwalimu ili tuwe wazalendo katika nchi yetu na tufanye kazi tupate maendeleo’ ,alisema Ng’ong’a 

Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Rafiki  SDO wamesema katika makumbusho hayo wamejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna Baba wa Taifa alivyoipenda nchi, huku wakisema kuwa wapo tayari kufuata nyayo za baba wataifa hasa katika utendaji kazi ili kupata maendeleo zaidi. 

Ziara ya Rafiki SDO mkoani mara ni sehemu ya kusheherekea siku ya rafiki na familia Rafiki Family Day

Angalia picha hapa chini
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakiwa katika kaburi la  Baba wa taifa  hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere mkoani Mara - Picha zote na Steve Kanyefu - Malunde1 blog
Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwongozaji wa wageni wanaofika katika makumbusho ya makazi ya baba wa Taifa bi. Gaudencia Waziri akitoa ufafanuzi juu makumbusho hayo kwa wafanyakazi wa Rafiki SDO.
Bi Gaudencia Waziri akitoa ufafanuzi katika makaburi ya wazazi wa hayati Mwalimu J.K Nyerere
Makaburi ya wazazi wa Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wafanyakazi wa Rafiki SDO wakicheza mchezo wa bao alilokuwa akicheza Hayati  Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wageni wake waliokuwa wakimtembelea enzi za uhai wake nyumbani kwake Mwitongo Butiama .
Moja ya picha kubwa inayopatikana katika makumbusho ya Mwalimu J.K Nyerere , picha hii inaonesha baadhi ya picha za Baraza la mawaziri la mwisho la rais wa kwanza Mwl. J.K Nyerere wakati akielekea kung'atuka madarakani mwaka 1985.
Mkurugenzi mtendaji wa Rafiki SDO, Gelard Ng'ong'a akitazama baadhi ya kumbukumbu zinazopatikana katika makumbusho hayo
Hii ni radio ambayo alikuwa akiitumia Hayati Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali ,hayati Mwalimu pia alipenda kutumia radio hii katika baadhi ya ziara  zake za ndani na nje ya nchi ,Redio hii alipewa nchini Ujerumani mwaka 1996.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Rafiki SDO Gelard Ng'ong'a akimsalimia  mtoto wa sita Hayati Baba wa taifa   Mwalimu  Nyerere, Madaraka Nyerere mara baada ya kutembelea makumbusho ya makazi ya baba taifa katika kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la  Rafiki SDO wakiwa katika picha ya pamoja mmoja ya watoto wa baba wa taifa , Madaraka Nyerere.

Picha zote na Steve Kanyefu - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post