Friday, November 30, 2018

WAFUASI WA CHADEMA WATIMULIWA MAHAKAMANI WAKIFUATILIA KESI YA MBOWE

  Malunde       Friday, November 30, 2018
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (Cuf) wametimuliwa na polisi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuanzisha kwa vurugu.

Tukio hilo limetokea mapema leo asubuhi Ijumaa Novemba 30, baada ya Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo ili kuwadhibiti wafuasi hao kutokana na kesi kubwa mbili zinazotarajiwa kutolewa uamuzi leo.


Kesi hizo ni pamoja na ile iliyofunguliwa na viongozi wa Cuf, wakitaka kujua Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, ni mwenyekiti halali wa chama hicho au la.


Kesi ya pili ile ya maombi ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko ambayo inatarajiwa kutolewa uamuzi kuhusu pingamizi lililowasilishwa na upande wa Jamhuri la kutaka rufaa itupwe ya kupinga kufutiwa dhamana kwa washtakiwa hao litupwe kutokana kutofuata vifungu vya kisheria.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post