Picha : BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WA NMB MKOA WA SHINYANGA

Benki ya NMB imeendesha mafunzo kwa Mawakala NMB mkoa wa Shinyanga kwa ajili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafahamu mbinu za kudhibiti fedha haramu pamoja na mbinu za kukuza biashara zao kwa kuongeza wateja.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni alikuwa Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Melusori alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha mawakala kukuza kipato chao lakini pia namna ya kudhibiti fedha chafu/haramu ‘Money laundering’.

“Lengo jingine ni kuwasilisha na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili mawakala hawa,kuwapongeza/kutambua mchango wa mawakala wanaofanya kazi vizuri na kuwaeleza kuhusu maboresho yanayofanywa na NMB”,alisema Melusori.

Hata hivyo aliwataka mawakala wa NMB kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria halali za fedha.

“Asilimia ya watanzania wanaotumia benki ipo chini ya asilimia 20 kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni hivyo shirikiane na benki kuhakikisha kuwa watanzania ambao hawajaanza kutumia huduma ya benki kwani benki ni sehemu salama zaidi”,aliongeza.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah alisema benki ya NMB yenye matawi 228,ATM mashine 715 ina mawakala 7000 wa NMB nchini kati yao 75 ni wa mkoa wa Shinyanga.

“Nawapongeza mawakala wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa NMB,tunajivunia sana kuwa na mawakala waadilifu,tumeamua kuwafikia kwani tunajali wateja wetu kwani lengo letu ni kutoa huduma bora,salama na zenye ufanisi”,alisema.

Alisema katika mafunzo hayo,miongoni mwa mada zilizotolewa ni pamoja na huduma zinazotolewa na NMB,Mawakala wa NMB,matumizi sahihi ya mashine za kutolea huduma,namna ya kupata mikopo na mbinu za kutambua na kudhibiti watakatishaji wa fedha ‘watu wabaya’.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mada ukumbini.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya NMB.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akiendelea kutoa mada ukumbini.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mada ukumbini.

Mafunzo yakiendelea.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na wakala wa NMB.

Mawakala wakiwa ukumbini.

Mafunzo yanaendelea.

Wakala wa NMB,Johari Ibrahimu akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Mikopo benki ya NMB Manonga,Magreth Mbuduka akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya mikopo katika benki hiyo.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mafunzo hayo.

Mafunzo yanaendelea.

Mafunzo yanaendelea.

Wakala wa NMB Kasiano Kicho akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akielezea kuhusu mambo ya kuzingatia katika biashara ya uwakala.

Afisa wa Benki ya NMB Richard Paul akielezea kuhusu huduma zinazotolewa na mawakala wa NMB .

Msimamizi wa Sheria,Taratibu na Kanuni benki ya NMB Kanda ya Tabora, Janeth Uiso akitoa mada jinsi ya kuzuia vitendo vya kutakatisha fedha na kuwezesha kifedha vikundi vya kigaidi.

Msimamizi wa Sheria,Taratibu na Kanuni benki ya NMB Kanda ya Tabora, Janeth Uiso akiwataka mawakala wa NMB kujiepusha na vitendo vya kutakatisha fedha.

Wakala wa NMB Joeli Fanueli Moshi akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Mauzo/Huduma Mbadala benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Trifon Melkiory akitoa mada kuhusu matumizi ya mashine za kutolea huduma
Afisa Mauzo/Huduma Mbadala benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Trifon Melkiory akitoa mada kuhusu matumizi ya mashine za kutolea huduma.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mada ukumbini.
Kushoto ni Meneja wa mauzo benki ya NMB Manonga, Thadei Mhengilolo na Afisa Mdhibiti ubora wa benki ya NMB,Timotheo Elias wakiwa ukumbini.
Wakala wa NMB,Juliana Shilatu wa mjini Shinyanga akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo.

Wakala wa NMB,Magese Lusambagula Shagembe kutoka Solwa akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Mdhibiti ubora wa benki ya NMB,Timotheo Elias akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Wa pili kushoto ni Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akimtangaza Juliana Shilatu (wa kwanza kulia) kuwa ni Wakala Bora wa NMB mkoa wa Shinyanga wakati wa kutangaza mawakala 10 bora wa NMB mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2018.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi zawadi ya cheti na fedha taslimu 100,000/- bi Juliana Shilatu aliyetangazwa kuwa Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga,Juliana Shilatu akielezea mbinu mbalimbali anazotumia kufanya kazi ya uwakala.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Saha Dachi and Company shilingi 75,000 mshindi wa nafasi ya pili ya wakala bora wa NMB.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Amos Francis Ndila shilingi 60,000 mshindi wa nafasi ya tatu ya wakala bora wa NMB.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Ngenda Mabula Hamis shilingi 50,000 mshindi wa nafasi ya nne ya wakala bora wa NMB.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Hamis Ahmad mwakilishi wa Micatel Tanzania Ltd shilingi 50,000 mshindi wa nafasi ya tano ya wakala bora wa NMB.

Mawakala wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini.


Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mafunzo yanaendelea.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527