MAHAKAMA YAAGIZA FREEMAN MBOWE,ESTHER MATIKO WAKAMATWE


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeagiza kukamatwa kwa washtakiwa, Freeman Mbowe na Esther Matiko kwa kutofika mahakamani kusikiliza kesi yao na viongozi wengine wa CHADEMA hii leo kinyume na masharti ya dhamana.


Kesi inayowakabili viongozi wakuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imeendelea kusogezwa mbele baada ya aliyekuwa wakili waanayemtetea Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Petter Msigwa Wakili Jamhuri Johnson kutangaza kujiondoa.

Uamuzi wa kujiondoa kwa wakili wa Msigwa ambaye ni miongoni mwa washtakiwa makosa mbalimbali kwenye kesi hiyo umetokana na kile alichokidai kuwa haridhishwi na mwenendo wa kesi hiyo akisema kuwa katika miaka 20 ya uwakili wake, hakuwahi kuona kesi inaendeshwa kwa namna hiyo.

Awali, washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali lakini waligoma kujibu lolote kwa madai ya kuwa kutokuwepo kwa wakili wao. Kwa upande wake mdhamini wa mshtakiwa wa kwanza, Freeman Mbowe, ameieleza mahakama kuwa bado yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Viongonzi wakuu wa Chama hicho wanakabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuhamasisha uchochezi na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Taifa (NIT), AkwIlina Akwilini wakati wa uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia alimshinda aliyekuwa mgombea wa CHADEMA, Salum Mwalimu.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527