EMMANUEL MBASHA AKERWA JINSI ROSE MUHANDO ALIVYOTOLEWA MAPEPO

Kuna video imesambaa ikimuonyesha Mwimbaji Mkongwe wa nyimbo za Gospel Rose Muhando akifanyiwa maombi ambapo kila mmoja amekuwa na maoni yake baada ya kuitazama. Hapo chini ni mtazamo wa Msanii wa Injili, Emmanuel Mbasha.


'Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kuweka wazi kuwa nimehuzunishwa sana na hii video ya maombezi ya muimbaji mwenzetu Rose Muhando.


Kwa unyenyekevu kabisa naweza kusema kuwa, maombi ni muhimu sana kwa watu wote, ila namna ya kuombea ikiwa mbaya inaweza kuharibu umuhimu wote wa maombi na kusababisha maombi yadharaurike au yamdharaulishe aliyeombewa.


Katika nia yangu ya ndani nimefurahishwa sana na kitendo cha Rose kuombewa, ila kero yangu kubwa imekuwa kwenye njia iliyotumika kumuombea. Rose Muhando ni star, na katika medani za mziki wa injili ni mtu anaetazamwa na watu wengi sana kama rol model wao, hivyo nadhani ilikuwa ni bora zaidi kuwa waangalifu katika kumuombea ili kulinda brand yake.


Biblia inasema, mwenye heshima apewe heshima, hivyo kwangu mimi sidhani kama mchungaji aliyemuombea Rose amempatia heshima anayostahili, maana binafsi sikuona haja ya kuwasha camera na kuanza kumuombea hadharani vile.


Hali hii inaweza kumtangaza sana muombeaji lakini kwa upande wa muombeaji inaweza kuzidisha tatizo na kusababisha adharaulike zaidi kwenye jamii inayomtazama. Watumishi wa Mungu mahitaji kuwa na hekima pamoja na kifua cha kutunza siri, na siyo kufanya mambo kwa mihemko huku mkitazama maslahi yenu.


Mimi nadhani ingekuwa bora sana endapo mchungaji angemuombea ofisini, na kama maombi yangeleta majibu naamini video ya shuhuda ambayo Rose Muhando ange ongea wakati akiwa na akili zake timamu ndiyo ingefaa kusambaa na kuendelea kumjengea heshima yeye pamoja na mtumishi aliyemuhudumia.


Kumbuka yule Akida (mkuu wa vikosi cha askari wa kirumi) alipohitaji maombi kwa Yesu, Biblia inasema Yesu alifunga safari kwenda nyumbani kwake ili kumuombea. Unadhani kwanini hakumwambia apelekwe amuombee hadharani kama alivyofanya kwa Batromayo? Hii ilikuwa ni hekima ya kulinda heshima ya muombewaji. Maana huwezi kumuombea Rais kama unavyoombea ombaomba au mpiga debe.


Kwa kweli nimeamua kuwa muwazi na kuziweka huzuni zangu hadharani ili waombeaji mjirekebishe. Siyo kila maombi yafanyike wakati caméra ziko on, kuna mengine ya kuzima camera na kuomba kwa staha ili kuendeleza uhai na kipawa'

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527