MAHAKAMA: UPELELEZI KESI YA ZITTO KABWE UMEKAMILIKA. | MALUNDE 1 BLOG

Monday, November 26, 2018

MAHAKAMA: UPELELEZI KESI YA ZITTO KABWE UMEKAMILIKA.

  Kanyefu       Monday, November 26, 2018

Upelelezi wa kesi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, umekamilika.


Hayo yamebainika leo Jumatatu Novemba 26, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.

Kesi ya Zitto iko mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi na imepangwa usikilizwaji wa awali Desemba 13 mwaka huu.

Inadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi ya chama cha ACT Wazalendo mshtakiwa akiwa katika mkutano huo kwa nia ya kuleta chuki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la polisi alitoa Maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Katika shtaka la pili, Kweka alidai kuwa siku na mahali hapo, Zitto Kijitonyama alitoa Maneno ya uchochezi ambayo yalikuwa na lengo lenye kuleta hofu.

Aidha Zitto anadaiwa Kutoa waraka kwa umma ukiwa na Maneno ya kichochezi kwa nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya polis
i.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post