MWANAUME AJIUA AKIDAI MTOTO BAADA YA KUTENGANA NA MKEWE


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mayunga Samwel mkazi wa Mtaa wa Mkudi Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza amekutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia shuka.

Marehemu huyo amejinyonga kwa kile kilichosadikika kuwa alikuwa akimtaka mwanae mwenye umri wa miaka 2 ambaye alikua ameondoka na mke wake baada ya wanandoa hao kutengana ila yeye alikua akimtaka mtoto huyo kwa miezi 11 ili aendelee kuishi naye.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mkudi Sebastian Mkunda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kabla ya kifo cha marehemu alikuwa na malalamiko ya kudai mwanae kutoka kwa mke wake waliokuwa wameachana kwa muda mrefu.

Siku moja kabla ya mauti kumkuta kijana huyo inadaiwa alikuwa akilalamika kwa majirani zake kuhusu kuwa mbali na mwanae baada yeye na mkewe kutengana.

Mwili wa marehemu Mayunga umechukuliwa na jeshi la Polisi kwaajili ya Uchunguzi zaidi.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527