Tuesday, November 27, 2018

AJALI YAUA WATU 15 TARIME

  Malunde       Tuesday, November 27, 2018

Moja ya gari lililopata ajali na kuteketea kwa moto Tarime.

Takribani watu 15 wamefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto kufuatia ajali  iliyotokea katika eneo la Komaswa maarufu kama kwa Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kuzikutanisha gari mbili za abiria aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na kisha kuteketea kwa moto.

Henry Mwaibambe, kamanda wa jeshi la polis kanda maalum Tarime Rorya akizungumza akiwa katika eneo la tukio ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa bado hakijajulikana lakini dereva wote kwenye ajali hiyo wamepoteza maisha.

“Kuna watu wengine ambao hawajatambuliwa, tunajitahidi ili watambuliwe, chamsingi ambacho hakina ubishi madereva wote wamefariki, lakini tunaendelea na uchunguzi ili kujua idadi kamili ya watu waliofariki hatuwezi kuwaficha marehemu,” amesema Kamanda Mwaibambe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime Bw. Glorius luoga ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuwataka madreva kuwa makini pindi wanapokuwa wamebeba abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post