MTOTO WA MWIGIZAJI MAARUFU DUNIANI AOA MWANAMKE MWENZIE


Mtoto pekee wa kike wa muigizaji maarufu wa filamu duniani, Jackie Chan, anayejulikana kwa jina la Etta Ng, amethibitisha kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye ni mwanamke mwenzake, anayejulikana kwa jina la Andi Autumn.

Etta ambaye ana umri wa miaka 19, alipost picha kwenye mtandao wa kijamii huku akiandika ujumbe wa mahaba na upendo wenye hashtag inayozungumzia ndoa za jinsia moja, huku wakionyesha cheti chao cha ndoa.

Kwenye ujumbe huo ambao umepostiwa na Etta, baadhi ya sehemu unasema, “kila mmoja anastahili upendo na mpaka pale nilipohisi upendo, naweza kuwa na uhakika kwamba maelewano, muunganiko, na upendo kwenye uso wa chuki, unaweza ukaponya nafsi iliyopotezwa, upendo hushinda”.

Wawili hao ambao walifunga ndoa nchini Canada ambako ndiko nyumbani kwa Andi, kwa sasa wapo Hong Kong ambako ni nyumbani kwa Etta.

Taarifa zaidi kutoka Hong Kong zinasema kwamba Baba mzazi wa Etta ambaye ni Jackie Chain yuko sawa na binti yake kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, lakini wawili hao hawana mawasiliano ya mara kwa mara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post