Picha : MABINTI TGGA TEMEKE WAPINGA NGONO, MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI


Girl Guides wa Wilaya ya Temeke, wakikataa ndoa na mimba za utotoni wakati wa maadhimisho a Siku ya Mtoto wa Kike yaliyoandaliwa na uongozi wa TGGA Temeke, kwenye Ukumbi wa Idd Nyundo Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam. Katikati aliyevaa miwani ni Mgeni rasmi Mwalimu Hawa Chanafi wa Shule ya Tandika. Chanafi alimwakilisha Meya wa Temeke.

TGGA Temeke hadi sasa ina wanachama 5200. Tamasha hilo lilihudhuriwa na wanafunzi kutoka shule za Wailes, Likwati, Keko Magurumbasi, Tandika, Chamazi na Uwanja wa Ndege.
Kamishna wa Tanzania Girl Guides Association -Temeke, Komba (kushoto) , akiwa na Mgeni rasmi, Hawa Chanafi pamoja na Mwenyekiti wa TGGA Temeke, Mary Gabusa wakipiga makofi wakati wa maadhimisho hayo.
Girl Guides wakiwa na bango lenye ujumbe wa Nguvu ya Mtoto wa Kike
Wakiimba wimbo wa Taifa
Kamishna wa TGGA Temeke, Komba akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ya Mtoto wa Kike ya Kupinga ndoa na mimba za utotoni.Komba aliwataka mabinti ili kutimiza malengo yao muda wote wajilinde dhidi ya watu wabaya wanaotaka kuwaharibia maisha yao
Girl Guides wakifurahi
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamazi, wakitumbuiza kwa wimbo wa Taarabu
Mabinti kutoka Shule ya Msingi Chamazi Dar es Salaam, wakitumbuiza kwa ngoma yenye maudhui ya kukataa ngono, mimba na ndoa za utotoni
Wanafunzi wakiigiza kwa kumkamata na kumpeleka Polisi mwanafunzi aliyeigiza kama baba ambaye alikuwa analazimisha kumuozesha kwa mzee mtoto wake ambaye ni mwanafunzi
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakiigiza kusikitika jinsi baadhi ya wanaume wanavyotoa vishawishi kwa watoto wa kike kwa lengo la kufanya nao ngono na kuwapatia mimba.
Girl Guides kutoka Shule ya Msingi Wailes wakifanya shoo ya mitindo ya mavazi
Mgeni rasmi, Chanafi akihutubia katika maddhimisho hayo ambapo aliwaasa watoto wa kike kukataa ngono,mimba na ndoa za utotoni ili watimize ndoto zao za maishao yao ya baadaye.
Chanafi akisisitiza jambo kwa kuwaambia watoto wa kike wasikubali kulaghaiwa na mtu yeyote kufnya nao ngono za utotoni ili wasonge mbele kimaisha
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maadhimisho kumalizika
Mgeni rasmi akiagana na Girl Guides

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527