Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI MKOA WA SHINYANGA YAFANYIKA BUNAMBIYU..SHUHUDIA KILA KITU HAPA


Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Bunambiyu kata ya Bunambiyu wilaya ya Kishapu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za watoto.

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la kuhudumia watoto la Save The Children kwa kushirikiana na shirika la Agape yamefanyika leo Alhamis Oktoba 11,2018 katika Senta ya Bunambiyu ambapo mgeni rasmi alikuwa Joseph Swalala kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kishapu.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani mwaka huu ni “Imarisha uwezo wa mtoto wa kike; Tokomeza ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni”.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo,Mgeni rasmi Joseph Swalala aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuwapatia watoto haki ya elimu badala ya kuwaozesha huku akisisitiza kuwa kuozesha mtoto wa kike ni kujipatia laana tu.

Swalala alisema jukumu la kulinda watoto ni la jamii nzima hivyo ni vyema kila mmoja akachukua hatua pale anapoona mtoto anakatishwa masomo.

Aidha aliwataka maafisa watendaji kutokaa na mashauri ya kesi za mimba na ndoa za utotoni kwenye ofisi zao badala yake wayapeleke mara moja polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Akisoma risala kwa niaba ya Watoto wa kike,Magreth Julius alisema maisha duni katika familia kimekuwa chanzo kikubwa cha wazazi kukatisha watoto masomo na kuwaozesha huku mila na desturi kandamizi zikiendelea kuendekezwa katika jamii.

Aliomba watoto wajengewe uwezo wa kujiamini kwa kuwapatia elimu ya kujitambua sambamba na kuweka mkazo kwa elimu ya afya ya uzazi.

Naye Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema shirika hilo katika kutekeleza mradi wa Kupambana na Mila na desturi kandamizi kwa mtoto wa kike,wamebaini kuwa changamoto ya ndoa na mimba za utotoni bado ni kubwa wilayani Kishapu.

“Tumegundua kuwa wilaya ya Kishapu ndiyo inaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga hali inayochangiwa na baadhi ya wazazi kuendekeza mila na desturi zisizofaa ikiwemo kuozesha watoto na kuwakatisha masomo”,alieleza Malima.

Alibainisha kuwa ukosefu wa mabweni pia ni changamoto kwani wanafunzi wamelazimika kupanga ‘gheto’ na vijana wa uraiani wanatumia fursa hiyo kuwaweka kinyumba wanafunzi wa kike.

“Vijana hawa wanalala na wanafunzi, halafu kesho mwanafunzi anaingia darasani,tunaomba serikali yetu sikivu inayoongozwa na rais Magufuli ituangalie watu wa Shinyanga kwa jicho la pekee kwani hatutaki kuongoza kwa mimba na ndoa za utotoni”,alisema Malima.

Aidha Malima aliwataka wazazi kuwa na ushirikiano na walimu katika kulea watoto huku akisisitiza kuwa watoto wote ni sawa hivyo wasibaguliwe.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mgeni rasmi Joseph Swalala akiwahutubia wakazi wa Bunambiyu na wadau mbalimbali wa haki za watoto leo Oktoba 11,2018 wakati wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Bunambiyu wilayani Kishapu.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mgeni rasmi Joseph Swalala akiwahutubia wakazi wa Bunambiyu na wadau mbalimbali wa haki za watoto leo Oktoba 11,2018 wakati wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Bunambiyu,Elisha Simon,kulia ni Diwani wa kata ya Bunambiyu Richard Sangisangi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Kishapu Rehema Edson akitoa neno la utangulizi wakati wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani na kuwataka wazazi na walimu kushirikiana kulinda na kulea watoto.Kulia ni Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa Shirika la Agape Peter Amani na akifuatiwa na Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa Shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga Msemakweli Bitangacha.
Wakazi wa Bunambiyu wakimsikiliza Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga,Benety Malima.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati wa wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani. Kulia ni Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa Shirika la Agape Peter Amani,kushoto ni diwani wa kata ya Bunambiyu,Richard Sangisangi.
Kushoto ni Mwanafunzi Magreth Julius akisoma risala kwa niaba ya watoto.
Diwani wa kata ya Bunambiyu Richard Sangisangi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambapo alikiri kuwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni lipo katika kata hiyo na kuwataka wadau wote kushirikiana ili kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto zao.
Vijana wanaolelewa na Shirika la Agape la Mjini Shinyanga wakiimba wimbo kuhusu changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike na kusababisha washinde kutimiza ndoto zao. Vijana hao ambao ni wahanga wa ndoa na mimba za utotoni waliimba kwa huzuni huku wakitokwa machozi hali iliyosababisha baadhi ya wadau waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani kutokwa machozi.
Wanafunzi wa shule mbalimbali katika kata ya Bunambiyu wakisikiliza wimbo wa vijana kutoka shirika la Agape.
Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima,akifuatiwa na Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa Shirika la Agape Peter Amani na Afisa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa Shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga Msemakweli Bitangacha.
Wadau wakiwa eneo la tukio.
Wakazi wa Bunambiyu wakiwa eneo la tukio.
Afisa Mtendaji wa kata ya Bunambiyu Thomas Nyonyo akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa kijiji cha Bunambiyu,Elisha Simon akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika katika kijiji chake.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani mkoa wa Shinyanga pia yaliambatana na Maandamano ya wanafunzi wa shule mbalimbali zilizopo katika kata ya Bunambiyu wilayani Kishapu na wadau mbalimbali wa haki za watoto: Wanafunzi wakiwa wameshikilia bango lenye ujumbe 'Jamii linda mtoto wa kike,mtoto wa kike wa mwenzio ni wako.
Wanafunzi wakiwa katika maandamano huku meza kuu ikiwa imesimama kupokea maandamano hayo.
Vijana kutoka shirika la Agape hawakuwa nyuma wakati wa maandamano hayo,nao wakajitokeza na mabango yao.
Vijana kutoka Klabu za Tuseme zilizoundwa na shirika la Save The Children na Agape nao walikuwepo kwenye maandamano hayo.
Wanafunzi wakiendelea kuandamana na mabango yao.
Wanafunzi wakiendelea kuandamana.
Vijana wa skauti kutoka shule ya sekondari Bunambiyu nao walinogesha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.
Wanafunzi wakiendelea kuandamana.
Kila bango na ujumbe wake...
Kikundi cha Nyuki cha TGNP nacho kilikuwepo kwenye maandamano.
Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Wakazi wa Bunambiyu wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.
Wanafunzi wakiimba wimbo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bunambiyu wakicheza ngoma ya asili maarufu 'Wigashe'.
Wadau wakiendelea kufuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Kikundi cha Mtandao wa nyuki 'TGNP' kikionesha igizo kuhusu ndoa za utotoni.
Wanafunzi wakionesha mchezo kuhusu tofauti kati ya mtoto wa kike na mtoto wa kiume.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yakiendelea.
Vijana kutoka shirika la Agape wakicheza ngoma za asili.
Akina mama wakazi wa Bunambiyu wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani leo Oktoba 11,2018.
Akina mama wa Bunambiyu wakicheza muziki wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.
Kikundi cha wakulima Mwamaditi  kikitoa burudani ya ngoma za asili
Msanii Jemedari Toto la Kisukuma na kundi lake wakitoa burudani.
Burudani inaendelea..
Mratibu wa CHF wilaya ya Kishapu Abednego Madole akihamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii ‘CHF iliyoboreshwa’.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post