MCHUNGAJI MSIGWA KUMBURUZA MAHAKAMANI MKUU WA MKOA WA IRINGA ALLY HAPI

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema atamfikisha mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kufuatia uamuzi wake wa kumuweka ndani diwani wa Viti maalum CHADEMA, Silestina Jonso.


Msigwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa jana Octoba 2, alisema Hapi alimdhalilisha diwani huyo.


“Alidiriki kumdhalilisha diwani wetu, sheria iko wazi sana, vipengele vyote vile mkuu wa mkoa hakufuata, amekiuka, ametoa amri ya kumpeleka diwani wetu polisi kinyume cha sheria.


“Sasa kwa sababu amekiuka taratibu, mimi kama mwenyekiti wa kanda na mbunge ili kukomesha tabia hii ya RC Hapi tumwambie hatukubaliani naye na hatujalala, anakuja na sheria zake za kutisha watu na kuwatia ndani.


"Tumejipanga vizuri tunamfungulia kesi mahakamani kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya. Tutakutana naye mahakamani kwa sababu anatumia madaraka vibaya.” Alisema Msigwa
Theme images by rion819. Powered by Blogger.