SHULE 10 NA WANAFUNZI 10 BORA KITAIFA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2018

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetaja shule 10 bora kitaifa zilizofanya vizuri katika matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi, huku mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa ikitoa shule sita katika orodha hiyo.Shule hizo ni Nyamuge (Mwanza), Twibhoki (Mara), Kwema Modern na Rocken Hill (Shinyanga), Jkibira, St Achileus Kiwanuka, St Severine na Rweikiza (zote Kagera).


Shule iliyoshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora ni Raskazone ya Tanga huku St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam ikishika nafasi ya sita.


Pia, wanafunzi sita kati ya 10 waliofanya vyema kitaifa katika mtihani huo pia wanatokea shule za kanda ya ziwa.Dk Msonde amewtaja watahiniwa 10 bora kitaifa na shule zao kwenye mabano ni Ndemezo Lubonankebe (Kadama-Geita), Innocent Seleli (Carmel-Morogoro), Given Malyango (Tumaini Junior –Arusha), Diomedes Mbogo (St Achileus Kiwanuka-Kagera), Sweetbert John (Mingas-Shinyanga).


Najma Manji (Nyamuge-Mwanza), Beatrice Jeremiah (Mapinduzi B-Mara), Mohamed Abdirahman Mohamed na Luqman Ally (Raskazone-Tanga) na Francisco Maiga (Kadama-Geita).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post