DAR YANG'AA MATOKEO DARASA LA SABA...MAKONDA AWAPONGEZA WALIMU NAMBA MOJA KITAIFA

Kufuatia Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la Saba, Mkuu wa mkoa huo Mhe. Paul Makonda amewapongeza Walimu,maafisa elimu, waratibu elimu, wazazi na wanafunzi kwa kuunganisha nguvu na kuifanya Dar es salaam kuendelea kuibuka kidedea.Makonda ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuahidi kutoa zawadi kama motisha kwa Walimu.


“Nawapongeza sana sana Walimu, waratibu kata, maafisa Elimu , wazazi pamoja na wanafuzi Kwa kuunganisha nguvu na hatimae tumeongoza ktk matokeo ya darasa la saba Tanzania.


"Asanteni sana kwakunivisha nguo na kumpa heshima Rais wetu Mpendwa. Ofisi yangu itaandaa utaratibu wa kutowa zawadi kama motisha na Asante Kwa kazi wanayoifanya walimu pamoja na wanafunzi. Tumeongoza tena kwa mara nyingine tena,“ameandika Makonda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527