IGP SIMON SIRRO AONGOZA MAZISHI YA IGP MSTAAFU SAMWEL PUNDUGU JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu Mji Mwema Kigamboni ambapo alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wastaafu,(kulia) na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wakati wa mazishi ya IGP mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Askari Polisi wakishiriki kushusha mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu kaburini wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu baada ya mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).

Maofisa wa Polisi nchini wametakiwa kumcha Mungu na kutenga muda wao katika kuhudhuria nyumba za ibada Misikitini na Makanisani jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi zao kwa kutenda haki kwa raia wanaowahudumia. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro jijini Dar es Salaam wakati alipowaongoza waombolezaji katika mazishi ya IGP Mstaafu Samwel Pundugu aliyefariki mwishoni mwa wiki na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni. 

Kwa Upande wake Mchungaji Andrew Fabian wa kanisa la KLPT aliyeongoza ibada ya mazishi hayo amewataka wanadamu kujiandaa mapema kwa kuwa hapa duniani siyo makazi yao bali ni wapitaji tu. 

Nao baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na marehemu wametoa wasifu wake huku wakisema alikuwa ni mtu aliyependa kazi yake na aliifanya kwa moyo kwa lengo la kuwasaidia Watanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post