WAZIRI MWAKYEMBE AHITIMISHA MASHINDANO YA DOTO CUP 2018 BUKOMBE


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amekabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya “Doto CUP 2018” yaliyofikia tamati jana katika uwanja wa shule ya msingi Uyovu, wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Kwa upande wa soka (wakubwa), timu ya Ushirombo Renjaz (Rangers) iliibuka mshindi baada ya kuichabanga timu ya Lyamba Mgongo bao 2-0 na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano, jezi seti tatu, mipira mitatu pamoja na kombe.

Mshindi wa pili timu ya Lyamba Mgongo ilijinyakulia shilingi laki tatu, jezi seti mbili na mipira mitatu huku mshindi wa tatu timu ya Kazibizyo FC akijinyakulia shilingi laki mbili, jezi seti moja na mpira mmoja.

Kwa upande wa watoto, timu za Simba na Yanga zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 na hivyo kila timu kujinyakulia shilingi 25,000 huku mfungaji bora Carol Frances na mlinda mlango bora Casto Paul wote wakiibuka na shilingi elfu hamsini kila mmoja.

Michezo mingine ilikuwa ni kuvuta kamba ambapo kwa upande wa wanaume Simba waliibuka mshindi dhidi ya Yanga na kujinyakulia shilingi elfu hamsini huku upande wa wanawake Yanga wakiibuka washindi dhidi ya Simba na kujishindia shilingi elfu hamsini pia.

Kwenye mchezo wa Karate, Shotokan walijishindia elfu hamsini, mpira wa wavu PVC walijishindia elfu hamsini, mbio za mita 100 wanaume mshindi alikuwa Projestus Rutha na wanawake ushindi ulienda kwa Tumain Mwasilembo ambapo kila mmoja alijinyakulia
shilingi elfu hamsini, mpira wa pete timu ya Kurugenzi alijinyakulia pia shilingi elfu hamsini.

Mbio za baiskeli mshindi mshindi wa kwanza Furaha Joseph alijinyakulia elfu sitini na mshindi wa pili Subi Kachila akijishindia shilingi elfu 40, mbio za magunia upande wa wanaume mshindi alikuwa Daniel Ishike na wanawake alikuwa Linda Deo ambapo
kila mmoja alijishindia shilingi elfu hamsini huku mbio za kuku wanaume na wanawake kila mshindi akiondoka na kuku.

Akizungumza kwenye fainali za mashindano hayo, Waziri Dkt. Mwakyembe alikiri suala la ubovu wa viwanja vya michezo katika halmashauri mbalimbali nchini ikiwemo Bukombe na kutoa
rai kwa halmashauri kuweka mikakati ya kuboresha viwanja hivyo na kwamba serikali itaunga mkono juhudi hizo ili kuhakikisha vinakuwa bora kwani michezo ni ajira.

Mashindano hayo yalianza Julai 27, 2018 yakiandalia na mbunge wa jimbo la Bukombe, Doto Mashaka Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini yakiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji, kuchochea maendeleo na kuimarisha umoja huku
kaulimbiu ikiwa ni “Kusema na Kutenda”.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye fainali za mashindano ya Doto Cup 2018 ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Mwandaaji wa mashindano ya Doto Cup, Doto Mashaka Biteko ambaye ni mbunge wa jimbo la Bukombe na pia Naibu Waziri wa Madini akizungumza kwenye fainali za mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya Bukombe mkoani Geita, Mhe. Said Nkumba akitoa salamu zake kwenye fainali za mashindano hayo
Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu akitoa salamu zake
Mbunge wa jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba akiwasilisha salamu zake
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akikabidhi zawadi ya kombe kwa timu ya Ushirombo Rangers baada ya kuibuka mshindi wa kwanza
Washindi wakifurahia ushindi wao
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akikagua timu za mpira wa pete
Mwandaaji wa mashindano ya Doto Cup, Doto Mashaka Biteko ambaye ni mbunge wa jimbo la Bukombe na pia Naibu Waziri wa Madini akisalimiana na wachezaji Tazama BMG Online Tv hapa chini
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post