HIZI HAPA PICHA ZA DARAJA REFU ZAIDI DUNIANI LILILOZINDULIWA CHINADARAJA REFU ZAIDI CHINA LAZINDULIWA

 Rais Xi Jinping wa China leo, Jumanne amezindua daraja refu zaidi lililojengwa na kusanifiwa kwa miaka 15 na lenye urefu wa kilomita 55 huko Zhuhai, kusini mwa China.

Uzinduzi rasmi wa daraja hilo la Hong Kong-Zhuhai-Macao unadaiwa kuwa mradi uliochukua muda mrefu na uliokabiliwa na ugumu zaidi kwani umevuka bahari na ni mradi wa kwanza kujengwa mkoani Guangdong, Macao na Hong Kong.

Daraja hilo limefanikisha azma yake kwa mara ya kwanza katika kuunganisha barabara kati ya Zhuhai, Macao na Hong Kong, huku likipunguza muda wa usafiri kutoka Hong Kong hadi Zhuhai na Macao kutoka saa 3 hadi dakika 45.


SOURCE:AZAM TV
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post