Saturday, October 27, 2018

Donald Ngoma amvuta Chirwa Azam

  Unknown       Saturday, October 27, 2018


BAADA ya uongozi wa Azam FC kupitia kwa meneja wake, Philipo Alando kutoa nafasi ya kocha wao, Mholanzi Hans van Der Pluijm kumsajili aliyekuwa straika wa Yanga Mzambia, Obrey Chirwa endapo ripoti yake itampendekeza, kuna ushawishi umetolewa juu ya mchezaji huyo.

Ushawishi huo umetoka kwa straika wa Azam FC, Donald Ngoma ambaye amesema Chirwa ni chaguo sahihi kutua klabuni hapo.
Chirwa kwa sasa anadaiwa kuvunja mkataba na timu yake ya Nogotoom ya Misri kwa kile kilichodaiwa timu hiyo kushindwa kukidhi mahitaji yake kwenye mkataba, ikiwa ni miezi michache tangu alipoachana na Yanga, aliyoitumikia kwa misimu miwili mfululizo.

Alando amesema ujio wa Chirwa hapa nchini hauhusiani na suala lolote juu ya kusajiliwa na Azam FC isipokuwa anaenda kule kwa sababu ya uhusiano wake na Ngoma.
“Uwezo wa Chirwa uwanjani ni mkubwa na ni wazi ana uwezo mkubwa kufanya lolote na kila mtu angemtamani isipokuwa sisi kama uongozi hatujafanya naye mazungumzo zaidi ya kocha Hans na ndugu yake Donald,” alisema meneja huyo.
Musa Mateja, Dar es Salaam
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post