DKT KIGWANGALA, PROF.KABUDI WAKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala wamekutana na Balozi wa Uingereza Nchini Bi. Sarah Cooke kuongelea masuala mbalimbali yanayohusu Utunzaji wa Wanyamapori na Vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori.


Waheshimiwa Mawaziri na Balozi pia wameongelea kuhusu mkutano wa utunzaji wa wanyamapori na udhibiti wa biashara ya wanyamapori ulioandaliwa na Serikali ya Uingereza na unaotarajiwa kufanyika wiki hii jijini London.

Aidha, Mhe. Balozi Cooke ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwezesha ziara ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William iliyofanyika hapa nchini.
Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bi Sara Cook akifanya kikao na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla katika ofisi ndogo za Wizara hiyo Mpingo House jijini Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post