TAMBWE AREJEA NA KUVUNJA MWIKO WA YANGA KUTOIFUNGA SINGIDA UNITEDMshambuliaji wa Yanga Hamis Tambwe amerejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu na kuifungia Yanga magoli 2-0 dhidi ya Singida United.

Tambwe alifunga mabao katika dakika ya 29 na 45 na kuvunja mwiko wa Yanga kutotamba kwa Singida kwa msimu mzima uliopita.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikifikisha pointi 12 na kuwaacha watani zao wa jadi Simba walio na pointi 10 huku yanga akiwa nyuma kwa mchezo mmoja.

Kwa matokeo ambayo timu hizi zimepata ni chachu kwa kila timu kuelekea homa ya pambano lao la watani wa jadi septemba 30 Simba SC atakapomualika Yanga.

Na Magdalena Kashindye - Malunde1 blog
Theme images by rion819. Powered by Blogger.