SOKO LA MLANGO MMOJA JIJINI MWANZA LATEKETEA KWA MOTO


Moto usiojulikana chanzo chake umeteketeza soko la Mlango Mmoja jijini Mwanza leo alfajiri Septemba 28,2018.

Jitihada za kudhibiti moto huo unaoteketeza mabanda ya wafanyabiashara zaidi ya 1000 wa eneo hilo zinaendelea.

Magari ya zimamoto na uokoaji yanaendelea kuuzima moto huo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana ambaye yupo eneo la tukio amesema mpaka inafikia saa mbili asubuhi walikuwa wamezima moto huo kwa asilimia 90.

Mmoja kati ya wafanyabiashara wa soko hilo, Elias Wambura amesema huenda moto huo ukawa umesababishwa na mamalishe ambao wana tabia ya kuacha majiko yao yakiwa na moto kwa lengo la kuyakuta alfajiri na kuendelea na shughuli yao ya mapishi.

"Sina uhakika lakini kwa upande wa hao wa mama, wana tabia ya kufunika moto kwenye majiko ili wakija asubuhi, isiwape taabu kuuwasha," amesema Wambura.

Mwenyekiti wa masoko jijini Mwanza, Hamad Nchora amewapongeza wafanyabiashara wa soko la Mlango Mmoja kwa ushirikiano walio nao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post