DIWANI MWINGINE WA CHADEMA ATIMKIA CCMDiwani wa kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru kupitia (Chadema), Ndg. Wilson Nanyaro ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na chama a Mapinduzi CCM kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Nanyaro ni diwani wa kumi na moja katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kwa kipindi hiki kwa kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Ndg. Emanuel Mkongo amethibitisha kupata taarifa za kujiuzulu kwa Nanyaro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post