Picha : WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUWAZIKA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Jumapili Septemba 23, 2018 ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya kitaifa ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya MV nyerere iliyotokea Septemba 20 mwaka huu. 

Mazishi hayo yamefanyika katika kijiji cha Bwisya kilichopo kwenye Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. Pichani ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye moja ya makaburi 9 ya watu waliozikwa leo,Watu hao 9 ni kati ya  224 waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambapo wengine wamechukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwafariji wakazi wa Ukara
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kivuko cha MV Nyerere kikiwa ndani ya ziwa Victoria
Muonekano wa kivuko cha MV Nyerere majini


Theme images by rion819. Powered by Blogger.