Picha : MAZISHI YA WATANZANIA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

Miili ya watu tisa kati ya 224 waliofariki kwenye ajali ya Kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria Septemba 20,2018 imezikwa katika viwanja vya shule ya Sekondari Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. 

Kati ya hao tisa, miili ya watu wanne ni ile ambayo haikutambuliwa. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ameongoza mazishi hayo kitaifa. 


PICHA ZOTE KWA HISANI YA MWANANCHI


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema leo asubuhi Septemba 23,2018 kwamba wanaendelea kutoa taarifa zaidi za upatikanaji miili hiyo kadiri inavyopatikana.

Anasema baadhi ya maiti zilizokuwa zimezama chini ya maji, zimeanza kuibuka na kuelea na tangu alfajiri miili minne imeonekana na kuopolewa katika fukwe za Bwisya.

Amesema uchimbaji wa makuburi unaendelea kwa ajili ya maziko ya miili ambayo haijatambuliwa.

Akizungumzia mazishi hayo, Mongella amesema wapo marehemu waliotambuliwa na ndugu zao lakini wakaomba wazikwe katika utaratibu ulioandaliwa na Serikali. 

"Wanaotambua na kuwa tayari kuchukua miili ya ndugu zao kwa maziko ya kifamilia wanaruhusiwa. Serikali inatoa ubani wa Sh500, 000 kwa kila maiti inayotambuliwa na kuchukuliwa," amesema Mongella

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post